CHANZO CHA VITA VYA WENYEJI WA AFRIKA KUSINI NA WAGENI NI SERA MBOVU YA ELIMU AFRIKA KUSINI BAADA YA MKATABA WA UHURU YAANI FREEDOM CHARTER
Nikiwa Afrika Kusini pamoja na kusoma mambo mengi kwa muda huo swali kubwa ambalo nilitaka majibu yake lilikuwa ni kwanini vijana wa Afrika Kusini wanawabagua watu waliowakomboa. Swali hili lilitupwa kwa Profesa wetu wa Sosiolojia hapo Wits University lakini tukaingia pia mitaani na sehemu mbalimbali kusaka majibu kwa njia YA utafiti unaojulikana kama ethnographic method yaani utafiti wa kufanya kwa kushiriki na kwa kuona kinachoendelea.
Nilitembelea sehemu zote muhimu Johannesburg na pembezoni ikiwa ni pamoja na magereza YA zamani walikofungwa wapigania uhuru na hasa sehemu ilipotangazwa Mkataba wa Uhuru maarufu kama Freedom Charter we nye vipengele zaidi ya 10. Katika uchunguzi huo yafuatayo yalibainika:
1. Zaidi ya wafanyakazi milioni 3 kwenye migahawa na hotelini yaani hospitality industry wanatoka Zimbabwe kwa sababu Afrika Kusini hawana wazalendo wenye ujuzi huo. Kwanini hawana? Vuta subira.
2. Asilimia 60 ya wafanyakazi kwenye mashamba ya Wazungu wanatoka nje ya Afrika Kusini kwanini?. Kwa sababu vijana wao hawana ujuzi unaohitajika na pia bado wanaona ni utumwa kufanya Kazi kwenye mashamba ya Wazungu.
3. Asilimia 60 ya watumishi kwenye Sekta ya ujenzi wanatoka Msumbiji kwa kuwa hawana wataalamu wa faini hiyo wanaohitajika kuajiriwa.
4. Zaidi ya Asilimia 60 ya waajiriwa kwenye migodi wanatoka nje ya Afrika Kusini kwa sababu ya nchi jirani zenye kuzalisha wafanyakazi na uchumi wa nchi hizo kuwa mbovu.
5. Kazi nyingi Afrika Kusini zinahitaji ujuzi wa Diploma na Cheti kutoka kwenye vyuo visivyotoa shahada. Watoto wa Afrika Kusini hawapendi kusoma kozi hizo na siyo Sera inayotiliwa mkazo na nchi.
Kwanini Afrika Kusini ilifikia hapo? Tulibaini sababu zifuatazo kuwa zimefikisha Afrika Kusini hapo ilipofikia.
1. Freedom Charter ilipinga ubaguzi na ukaandaliwa Sera ya waafrika weusi wa Afrika Kusini kusoma katika vyuo vikuu vya wazungu hivyo mlango ukafunguliwa mtoto kusoma katika Chuo Kikuu chochote.
2. Freedom Charter haikufikiria kuwa ili nchi ikuze ajira, zaidi ya Asilimia 50 ya wahitimu wanapaswa kuwa na technical education yaani wakawa ni technicians wenye ujuzi ngazi ya Cheti na Diploma.
3. Technical and Vocational Education haikuwa Sera iliyotiwa mkazo Afrika Kusini isipokuwa mkazo ulikuwa kwenye elimu ya Chuo Kikuu na fedha nyingi zikaelekezwa huo na baada ya miaka 10 ya utekelezaji wa Freedom Charter, nchi ikajawa na wasomi wenye elimu ya vyuo vikuu huku Technical and Vocational Training ikiendelea kudharauliwa na kufifia hasa katika maeneo ya hospitality, ujenzi na kilimo maeneo yenye ajira nyingi kwa wageni.
4. Wazungu walipopanua ajira katika maeneo hayo, wakakosa wazalendo wenye ujuzi katika ngazi ya Certificate and Diploma. Wasomi wengi wakawa wa Shahada ambazo hazikuhitajika kwenye soko la ajira. Njia pekee ilikuwa ni kuajiri wageni wenye ujuzi unaotakiwa.
5. Hatua hii ya Afrika Kusini kuzalisha wasomi wasiohitajika kwenye soko ndo chanzo cha wazawa kuwaona wageni kuwa wanachukua ajira zao na kuanza kuwachukia.
6. Mazingira ya makuzi ya watoto Afrika Kusini yanachochea uhasama kwani bado wanafundishwa kuwaona wazungu kuwa ni watu wabaya na wakandamizaji waliowaua wazazi au mababu zao. Elimu ya kuishi kwa Amani na adui haipo Afrika Kusini. Lugha ya mawasiliano nayo ni tatizo kwani wanaweza kubaguana kwa koo. Vile vile sheria zao bado ziko dhaifu sana.
7. Niliambiwa japokuwa sikuithibitisha kuwa Freedom Charter utekelezaji wake katika Kipengele cha usawa wa kijinsia imesababisha matatizo makubwa Afrika Kusini kwani binti akipata ujauzito akijifungua mlezi wa mtoto anapata posho ya kumlea mtoto wakati mama yake akiwa shule. Utaratibu huu unawachochea wazazi kupenda watoto wao wazae halafu wawatunzie watoto wakiwa shule kwani watapata posho. Sikulithibitisha kabisa suala hili.
8. Kimsingi zaidi ya asilimia 60 ya Kazi zilizoko Afrika Kusini zinahitaji wahitimu wa elimu ngazi ya Cheti na Diploma yaani waliosomea Technical and Vocational Education wakati zaidi ya asilimia 60 ya vijana wa Afrika Kusini wana Academic certificates katika ngazi ya Shahada ambazo hazina ajira.
9. Walioshikilia Ajira Afrika Kusini ni Wazungu hivyo wanaweza katika maeneo ambayo wanaona kuna usalama zaidi na pia wanapowaajiri wageni misuguano mingi inapungua sehemu za Kazi.
Kwa msingi wa maelezo hayo, mfumo wa elimu ndiyo imewaweka wahitimu wa Afrika Kusini mahali walipo. Wanaona nafasi zao za ajira zimechukuliwa na wageni wakati hawana sifa na ujuzi wa kufanya Kazi hizo hata kama wageni wataondolewa. NI vigumu sana kwa Afrika Kusini kurudi kwenye reli mpaka waingie kwenye Mtaala na Sera wapunguze wasomi wa vyuo vikuu wahimize elimu katika ngazi ya Technical and Vocational Education. Pia wawabadilishe mawazo watoto wao kuona Kazi kwenye kilimo, hospitality industry na ujenzi kuwa ni Kazi za watumwa walivyotumikishwa wazazi wao. Hilo linahitaji nchi kujipanga upya ila kwa sasa twende na Kitabu nikipendacho cha "Things fall Apart"
MTANZANIA WAPILI AELEZA:
Ngoja niwape kidogo story ya hapa South Africa.
Ukifuatilia kiundani kuna ukweli kwanini Wazulu au raia wa mataifa mengine inaonekana wanabaguliwa na kuuwawa?
1.Sheria ya South Africa ya mauaji bado haijabadilishwa kutoka ile ya kaburu ya kwamba unaua mtu halafu unapelekwa Polisi wanakuja ndugu zako wakuwekea dhamana unarudi nyumbani unaendelea na kazi yako kesi inakwenda mahakamani sasa fikiria aliyekufa sio raia wa Nchi hii niambieni ni ndugu gani atoke labda Tanzania au Nigeria kuja kusimamia kesi?inasomwa mara 3 hakuna mlalamikaji basi inafutwa.
2.Hata sisi wageni tunatatizo kwa upande mwingine.Kwanza hawa watu tumewabadilisha utamaduni ambao hawakuwa nao mfano kuhonga mwanamke kwao ni kosa sasa sisi wageni tunahonga na hao wadada wanaanza kuwakataa kaka zao wanapenda wageni wao wanaita (Makwelekwele) na kaka zao nao hawakubali ukizubaa tu unapigwa bunduki tena nyumbani kwako.
3.Ukioa Mzulu inabidi usiwe na wivu kwani anaweza kuondoka nyumbani ijumaa akarudi j3 asubui na anakwambia kabisa alikua club?ukimpiga anakwenda kuwaita kaka zake wa kitaa wanakuja wanakupiga na wanachukua kila kitu ndani ndoa kwaheri haijalishi umezaa naye.
4.Serikali ya South Africa mtoto akizaliwa anaanza kulipwa ni kama laki na ishirini; 120,000 ya Tanzania mpaka afikishe miaka 18. Hapo Serekali inaachana naye na ndio wanaoleta vurugu kwani walizoea hela sasa kafikisha miaka 18 account yake inafungwa wanaingia mitaani.
5.Wanasiasa ni tatizo huyu Rais wa sasa kwenye Kampeni aliwaahidi kuwa akipata urais foreigners wote ambao wanafanya kazi ambazo wazawa wanaweza kufanya atawafukuza sasa hajawafukuza wananchi wanadai ahadi na hasemi chochote
6.Ndani ya South Africa kuna Majimbo ambayo Rais hana nguvu Mfano Kwazulu Natal kule Chief wao ndiye wanamskiliza akisema leo kavamieni maduka ya wageni na chukueni kila kitu ni mali yenu wanakwenda hilo nalo ni tatizo.
7.Wageni na sisi tuna tatizo hasa kuuza bangi na madawa ya kulevya vijana wengi sana hapa ni mateja na ndio vibaka wapiga watu risasi utakuta anapo kuomba hela cha kwanza mwangalie vizuri je hana cha moto?ukiona hana unamchunia tu ila jiridhishe kwanza au mpe tu hela ndogo tu kama buku tu ya Tz.
No comments :
Post a Comment