Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, October 14, 2019

16 wauwawa kwenye shambulizi la msikiti nchini Burkina Fasso!

Maafisa nchini Burkina Faso wamesema jana kuwa watu wenye silaha wamewauwa waumini16 na kusababisha taharuki katika eneo lenye hali tete kaskazini ya nchi hiyo baada ya kuvamia msikiti wakati wa ibada.

Shambulio hilo la siku ya Ijumaa kwenye msikiti mkuu wa mji wa Salmossi limedhihirisha changamoto zinazoikabili nchi hiyo kwenye mapambano yake dhidi ya wapiganaji wa itikadi kali.

Duru kutoka eneo hilo zimesema watu 13 walikufa papo hapo huku watatu zaidi walipoteza maisha baadaye kutokana na majeraha na majeruhi wengine wawili wapo kwenye hali mahututi.
Raia mmoja amesema watu wameanza kulihama eneo hilo hata baada ya kuwasili kwa wanajeshi zaidi waliopelekwa kuongeza nguvu baada ya mkasa huo.

Makundi ya haki za raia yamesema mashambulizi ya kuvizia ya wapiganaji wa itikadi kali tayari yamewauwa zaidi ya watu 1000 nchini Burkina Fasso.

No comments :

Post a Comment