Manager wa Kitivo cha Computer cha PBZ Ltd Bw. Khatib Pandu Buyu akizungumza na Ktv Tz siku chache nyuma.
Akizungumza na KTV TZ, Mkuu wa Kitivo cha computer kwenye Makao Makuu ya PBZ mjini Zanzibar Bw. Khatib Pandu Buyu, alisema kuwa majaribio yamefanywa kwenye wakala wa Mwanakwerekwe na Magereza na matokeo yake ni mazuri na kwahivyo benki ya Watu wa Zanzibar kwa sasa imo katika kujiandaa ili kuwa na wakala zaidi katika kila mji wa Zanzibar na Bara.
Bwana Buyu aliendelea kueleza kuwa machine kama 100 tayari sishafanyiwa setup na zipo tayari kutawanywa Tanzania nzima kwa wale watakaotaka kuwa wakala wa PBZ katika maeneo yao.
Maelezo zaidi yatatolewa hivi karibuni na benki hio kwenye website yake: www.pbzbank.co.tz
Wachunguzi wa mambo ya kibenki wa ZanzibarNiKwetu wanaiona hii kama ni hatua muhimu na nzuri sana katika kuboresha huduma za PBZ na katika kuwapunguzia shida na taabu wateja wa PBZ hasa katika mwisho wa mwezi.
Wachunguzi hao wanaendelea kueleza kuwa hatua hii ilikuwa ichukuliwe zamani sana kutokana na mateso wananchi walivyokuwa wakiyapata pale walipokuwa wakipokea mishara yao katika kila mwisho wa mwezi, hasa kwavile benki nyingi Tanzania siku hizi wanatumia njia ya uwakala badala ya benki hizo kufungua matawi yao wenyewe.
Tunaiomba benki yetu pia ifikirie kuanzisha mobile banking unit ili iwafikie wananchi wa Zanzibar katika kila corner ya nchi yetu.
Tunaitakia benki yetu ya Watu Wa Zanzibar (PBZ LTD) mafanikio zaidi na zaidi!
THE PEOPLE'S BANK, THE PEOPLE'S CHOICE!
KWA NJIA YA UWAKALA HALI KAMA HII YA KUSIKITISHA INAYOONESHWA KWENYE VIDEO CLIP YA HAPA JUU HAITOTOKEA TENA KWENYE MATAWI YA
PBZ LTD!
PBZ LTD!

No comments :
Post a Comment