
Ameyasema hayo akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Azimio na kuwataka mawakala wote kuhakikisha wanawalipa wakulima fedha zao kwa muda wa siku kumi na nne
"Ninatoa siku 14 kwa mawakala wote wanaonunua pamba kuhakikisha wanawalipa wakulima fedha zao pamba wamelima wao na watoto wao na wake zao kwanini msiwalipe ?"
Hata hivyo amemtaka waziri wa kilimo na mifugo Japhet Hasunga kuhakikisha wakulima hao wanapewa pesa zao kama alivyoagiza
Kwa upande wake Wazili wa Kilimo Japhet Hasunga amesema serikali imetenga bilion126 kwa ajili ya ujenzi wa ghala za kuhifadhia pamba na kati ya hizo mkoa wa katavi umepewa bilion 14.2 kwa ajili ya ujenzi wa ghala ya kuhifadhia pamba.
Mkoa wa katavi umekusanya takribani Tani elf 770 za pamba na Tan elfu 5 tayali zimeshanunuliwa na mawakala ambazo ni sawa na gunia72 za pamba.na mpaka sasa bilioni 6.3 Bado hazijalipwa kwa wakulima wa zao hilo.
Hata hivyo wakulima wa zao hilo wameishukuru serikali kwa kuruhusu mkoa wa katavi kulima pamba kwani nikilimo ambacho kimewasaidia kijiinua kiuchumi licha ya kuwepo kwa changamoto ya kucheleweshewa malipo yao.
Mkoa wa katavi ni miongoni mwa Mkoa wenye ardhi nzuri yenye rutuba ya kustawisha mazao na pía ni mkoa ulioshika nafasi ya nne kwa kuzalisha mazao ya chakula.
No comments :
Post a Comment