
Amesema Zanzibar inavivutio vingi sana vya utalii ila wazanzibar na watanzania walio wengi wamekuwa hawavifahamu hivyo atatumia musiki wake katika kuvitangaza ili watu wengi wapate kwenda kuvitembelea na kujifunza. Hayo ameyaeleza leo Septemba 21 katika Mkutano maalumu na Waziri wa Habari utalii na mambo ya kale Zanzibar,Mahmoud Thabit Kombo katika ukumbi wa mkutano wa Wizara hiyo iliyopo Kikwajuni Mjini Magharib Unguja.
Mutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali na Taasisi Binafsi zenye dhamana ya kukuza utalii visiwani humo.
Ali kiba alisema kuwa yeye kama mwanamuziki anajukumu kubwa la kutangaza vivutio vilivyopo Nchini vijulikane na watu wengi wapate kwenda kuvitembelea kwa lengo kujifunza.
“Nipo tayari kutumia musiki wangu kutangaza utalii uliopo Nchini kwa kuanza vivutio vingi na vizuri vilivyopo visiwani Zanzibar” alisema Msanii huyo.
Aliongeza kusema kuwa watu wengi hawavijui vivutio hivyo na wapo Nchini hivyo wanatakiwa kuwana tabia ya kwenda kutembelea wa lengo la kujifunza na kuona kwa Neema waliojaliwa katika nchi yao.
“Watu wamekuwa wakija Kwetu kutembea na kujifunza ila sisi tuliokuwa hapa tunashindwa kuja Zanzibar kuona ngome kongwe na maeneo mengine kwa kujifunza na hata kujiburudika” Alisema Ali Kiba.
Aliongeza kusema kuwa wananchi wanapotembelea maeneo ya kihistoria na vivutio hivyo kufanya hivyo watasaidia Serikali katika kuinua utalii uliopo Nchini kupiga hatua na kuwanufaisha wengi zaidi. Katika maelezo yake Ali Kiba aliwashauri wasanii wengine kuwa mabalozi wa kutangaaza utalii wa Nchi kutokana kuwa kazi zao zinafika mbali.
“Ni jambo la kujitolea na kuitangaza Nchi yako kimataifa, hivyo niwaombe wasanii wenzangu kupitia sanaa musiki kuwa mabalozi wa kutangaza utalii uliopo Nchini” alisema Ali Kiba.
Katika hatua nyingine Ali Kiba aliwashauri wazazi na walezi Nchini kuacha tabia ya kuwakataza watoto wao kuimba musiki kwani Usanii wa Musiki ni kazi kama kazi nyingine ambapo inawaingizia kipato na kuwainua vijana kiuchumi.
“Usanii ni kazi kama kazi nyingine kwa sasa tuache mitazamo ya kizamani kuwa msanii ni uhuni, kazi hii ya usanii inatuingizia kipato, tunalala na kuishi vizuri hivyo ukimuona mwanao ana kipaji usimkataze unatakiwa kumuongoza kuwa na nidhamu na kuijua dini yake”alisema Ali Kiba. Nae Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya kale Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kushirikiana na msanii huyo ili kutangaza vivutio vilivyopo Zanzibar vijulikane haraka zaidi. Alisema Serikali imekuwa ikifanya kazi kubwa katika kutangaza vivutio kama vile maeneo ya kihistoria na upekee wa mbuga za wanyama zilizopo Zanzibar hivyo kupitia msanii huyo vivutio hivyo vitapata kujulikana haraka.
“Nilipokutana na Ali Kiba nilimueleza mambo mengi kuhusu Zanzibar na kumuomba kati ya videoshoting atakayoifanya basi aifanye Zanzibar ii kutangaza mambo ya kale ambayo yapo Zanzibar na kujulikana kwa haraka watu” alisema Waziri huyo.
Alifahamisha kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo tayari kushirikiana na wasanii mbali mbali katika kutangaza utalii wa Zanzibar katika Anga za kimataifa.




No comments :
Post a Comment