dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, October 11, 2019

Ofisi ya Rais Mstaafu Kikwete yasikitishwa na habari hizi!


Ofisi ya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete imeeleza masikitiko yake kuhusu upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu kuhusu hotuba aliyoitoa Kikwete kwenye Kongamano la Kumbukizi ya Miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Imesema kuwa mada ya Kongamano hilo ilikuwa ‘Urithi wa Mwalimu Nyerere katika Uongozi, Maadili, Umoja na Amani katika Ujenzi wa Taifa’ na Rais Mstaafu alieleza kwa namna alivyomfahamu Mwalimu Nyerere kulingana na mada hiyo.


Ofisi hiyo imesema Rais Mstaafu Kikwete ameshangazwa na kusikitishwa kwa kujitokeza watu wanaopotosha ukweli kuhusu maneno yake na kuwepo wanaojaribu kumuwekea maneno wakidai eti alikuwa anawasema baadhi ya viongozi waliopo sasa.

Aidha, ofisi imeeleza kuwa hakufanya ulinganifu kati ya Mwalimu na Marais walifuata baada yake, waliostaafu na waliopo sasa pia hakutaja jina la mtu yeyote, hivyo kusikia kuwa Rais Mstaafu alisema mtu ni jambo linalosikitisha ni uzandiki, fitna na Uchonganishi

Mwisho, Rais Mstaafu Kikwete amesema alitegemea watu wamkosoe kwa aliyoyasema na si kumsingizia na pia amewataka watu wenye maoni yao wawe wajasiri na kuyasema na sio kujificha katika kivuli cha hotuba yake.


No comments :

Post a Comment