Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Mahamat ametoa mwito wa kuondolewa mara moja vikwazo dhidi ya Zimbabwe.
Taarifa iliyotolewa jana na Bw. Mahamat ni mwendelezo wa mwito aliotoa mwezi Februari kufuatia ziara nchini Zimbabwe, kuunga mkono taarifa ya pamoja iliyotolewa na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC.
Akiongea mjini Harare kwenye ufunguzi wa shughuli ya kupinga vikwazo dhidi ya Zimbabwe, Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema Zimbabwe imechoshwa na vikwazo haramu, na kutaka viondolewe haraka bila masharti.
Nchini Afrika Kusini wanachama wa Chama cha ANC waliandamana kwa pamoja na Wazimbabwe kupinga kuwekwa kwa vikwazo hivyo.
No comments :
Post a Comment