
Ikiwa ni siku chache baada ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano Dkt.John Pombe Magufuli kutoa agizo kwa uongozi wa TANAPA mkoani humo kuhakikisha wanachimba bwawa na kuweka maji ili kuwasaidia wanyama hao aína ya viboko ambao asili ya maisha yao wanategemea maji kwa kiasi kikubwa.
"Ninawaagiza TANAPA muhakikishe mnachimba bwawa na mlijaze maji kuwasaidia hawa viboko wanateseka sana, unapokamua ng'ombe mpe na majani sasa nyie mnategemea kuingiza kipato kupitia hawa viboko halafu hamuwajali".
Pía Magufuli amewataka TANAPA kuanzisha bucha la nyama pori ambalo watauza aína mbalimbali ya nyama ili kila mwananchi afaidike na kuwepo kwa Hifadhi mkoa kwake
Hata hivyo ametoa msamaha kwa vijiji 60 ambavyo vinapatikana ndani ya Hifadhi hio kuendelea kuishi katika maeneo hayo na kuwataka kutohavunja sheria.
Takribani vijiji 920 nchi nzima vilivyo ndani ya Hifadhi ya taifa vimepewa kibari cha kuendelea kuishi katika maeneo yao bila kusumbuliwa.
Hifadhi ya Taifa mkoa wa katavi ni Hifadhi ya nne yenye eneo kubwa na nihifadhi ambayo Bado haijabadilika asili yake licha ya kuwepo kwa migogoro baina ya wakazi wanaoshi maeneo jirani na Hifadhi kuwazuru wanyama wanaotembelea kalibu na makazi ya watu
No comments :
Post a Comment