Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson siku ya Jumatatu atazungumza na viongozi wa Ujerumani, Ufaransa na rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya katika jaribio la kuwataka viongozi hao waunge mkono mkataba wake Brexit.Hayo yameelezwa na gazeti la Times la nchini Uingereza likinukuu chanzo kinachofahamu mipango ya mazungumzo hayo.
Wakati wa mazungumzo hayo na Kansela Angela Merkel, rais Emanuel Macron na Jean Claude Junker, Johnson atawarai viongozi hao wamsaidie kupata mkataba wa Brexit wiki inayokuja au waridhie Uingereza ijitoe kutoka Umoja wa Ulaya bila makubaliano ifikapo Oktoba 31.
Wajumbe wa mazungumzo ya Brexit kutoka Uingereza na Umoja wa Ulaya, waliingia kwenye mazungumzo magumu ya mwishoni mwa juma kutafuta njia ya kuondoa mkwamo wa Brexit kuelekea mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya baadae wiki ijayo.
No comments :
Post a Comment