Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 13, 2019

Bunge lapitisha sheria ya mtu kujipima UKIMWI!

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha sheria inayotoa mamlaka kwa mtu binafsi kujipima mwenyewe Virusi vya Ukimwi (VVU).

Akizungumza na wanahabari baada ya kutoka katika vikao vya bunge jijini Dodoma leo Novemba 12, 2019 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile amesema sheria hiyo itasaidia kwasababu watu wengi hasa wanaume wanaogopa kupima.

Ndugulile amesema sheria hiyo imeruhusiwa katika maeneo mawili ambapo kwanza wameruhusu upimaji binafsi na pili kuruhusu upimaji kuanzia umri wa miaka 15.
“Tumeona changamoto mbili, kwanza wanaume kujitokeza kupima na pili takwimu zinaonesha kuwa maambukizi sasa hivi yamehamia kwa vijana ambapo asilimia 40 ya maambukizi mapya ni vijana na kati ya hizo asilimia 80 ni mabinti ndiyo maana Serikali imekuja na mapendekezo ya sheria na tunashukuru kwa kuwa bunge limepitisha.

“Tutaanza upimaji binafsi ambapo kabla ya hapo upimaji ulikuwa unafanyika katika vituo vya afya na watu wengi walikuwa waoga hivyo hii itasaidia watu kujipima wenyewe nyumbani na vipimo hivyo havitumii damu bali kuna sampuli zinatolewa kinywani,” amesema.

Akizungumzia kuhusu kuruhusu vijana wa miaka 15 kupima bila ridhaa ya mzazi ni kwasababu vijana wengi hivi sasa wanaanza mahusiano wakiwa wadogo jambo linalochangia maambukizi mapya.

Aidha amesema utaratibu huo utaanza Januari mwakani baada ya Rais Dk. John Magufuli kuridhia na vipimo hivyo vitakuwa vinatolewa katika maduka ya dawa; “wauzaji wa vipimo hivyo watapewa mafunzo kabla ya kuanza kuviuza ili kuhakikisha kunakuwepo na utunzaji wa kumbukumbu,” amesema Dk. Ngduulile.

No comments :

Post a Comment