
Takribani watu 28 wamefariki huko mashariki mwa DR Congo kutokana na ajali ya ndege iliyokuwa imebeba watu 18 wakiwemo rubani wawili na abiria 16 na wengine 10 ni wakazi wa eneo ambapo ndege ilianguka
Ndege hiyo ilianguka katika mji wa Goma, kwenye mtaa wa Birere wenye watu wengi karibu na mpaka wa DR Congo na Rwanda.
Vyombo vya usalama vinaendelea na uchunguzi ili kufahamu watu wangapi walikufa na wangapi walijeruhiwa
Zoezi hilo linafanyika kwa msaada wa wananchi wa mji huo ambao waendelea kupekua nyumba za majirani zilizo angukiwa na ndege hiyo ya kampuni ya Beesyby
Kampuni hiyo imekuwa ikifanya safari zake huko Kivu kaskazini ikisafiri kati ya miji ya Goma, Butembo na Beni.
No comments :
Post a Comment