
Tarehe 20/4/571 sawa na tarehe za kiislam mwezi 12 mfungo sita, mwaka wa tembo,siku ya jumaa tatu ktk mji wa Makka, alizaliwa kiumbe bora kuliko viumbe wote duniani, wanahistoria wanasema huyu kiumbe ndio kiumbe anaeonggoza kwa umaarufu, yani anashika nambari moja,
Anaitwa Muhammad Bin Abdillah Bin Abdul Mutwalib, (s, a, w)
Kila mmoja ana aina ya kumkumbuka Na kumuadhimisha kuzaliwa kwa kiumbe huyu bora Na mtukufu mbele ya mwenye zimungu(s,w), lakini Mimi binafsi napendelea nimuadhimishe mtukufu huyu kwa kukumbuka jinsi alivyo zaliwa kwa mujibu wa wanahistoria walivyo tuhadithia.
Baba yake na mtume (s, a, w) alipo muowa Bi Amina bint Wahabi, ilipita miezi michache Sana mzee huyu akawa amepata Safari ya kwenda sham (syria ) kwaajili ya kwenda kufanya biashara,
Mzee Abdillah alifanikiwa kwenda mpaka sham na na alifanya biashara zake vyema na baada ya kumaliza akiwa Na wafanya biashara wenziwe walianza Safari ya kurudi Makka,
ghafla mzee Abdillah alipata maradhi ya ghafla njiani na ilikuwa karibu kidogo Na mji wa madina na akazidiwa Mpaka akawa amefariki,
Wafanya biashara wenzake wakaona isiwe taabu wakaamua kumzika mzee Abdillah, na kwenda kutoa taarifa kwa Baba yayake mzee Abdul Mutwalib.
Lakini wakati mzee Abdillah anasafiri kibiashara alimuacha mkewe Mama Amina akiwa ana ujauzito wa Muhammad (s, a, w) ukiwa una miezi michache tumboni humo.
Basi Bi Amina na mkwewe mzee Abdul Mutwalib hawakuwa na chakufanya zaidi ilikuwa ni kukubaliana na matoke na mpango wa mwenyezimungu.
Bi Amina akiwa chini ya uangalizi wa mkwewe mzee Abdul Mutwalib aliulea ujauzito wake mpaka muda Na wakati ulipofika wa kuzaliwa kiumbe bora kabisa duniani ulipo fika.
Ndipo ilipofika tarehe 20/4/571 sawa na tarehe za kiislam mwezi 12, mfungo sita, mwaka wa tembo, siku ya jumaa tatu alizaliwa mtume Muhammad (s, a, w) katka mji wa Makka.
Mzee Abdul Mutwalib kwa furaha yaekuzaliwa kwa mtoto huyu bora ambae kwakwe ni mjukuu, alimchukua mtoto huyu na kuzunguka nae kwenye alkaaba huku akiwa Na furaha kubwa mno kumpokea mjukuu wake huyo.
Ikumbukwe kuwa Alkaaba ni nyumba ambayo ilikuwa ikiheshimika Sana toka enzi na enzi kwa wakaazi wa mji wa makka,
Muhammad (s, a, w) alipokuwa mtoto alikuwa mtoto bora na mwenye kupendwa na kila mtu na kila rika pale nyumbani kwa mzee Abdul Mutwalib, babu yake Na mtume.
Kitendo cha kuzaliwa mtume Muhammad (s, a, w) kulisababisha Mpaka baadhi ya watumwa kuachwa huru kwa Rehma na baraka za kuzaliwa kiumbe bora, Muhammad (s, a, w)
Mfano Baba yake mdogo mtume Abii Lahabi alimtoa mjakazi wake (mtumwa wake )na alimuacha huru, aliekuwa akiitwa Thuwaibat Aslaamiya na kumpeleka nyumbani kwa Baba yake mzee Abdul Mutwalib ili akasaidizane kwenye malezi ya kumlea Muhammad (s, a w).
Na huyu mjakazi Thuwaibat Aslaamiya ni miongoni mwa mwanamke aliemnyonyesha maziwa mtume kabla ya kunyonyeshwa na Halimat Saadia.
Ilikuwa ni furaha imeingia ndani ya nyumba ya mzee Abdul Mutwalib na ndugu jamaa majirani wote walijikuta wanamfurahia kiumbe huyu bora ktk ulimwengu,
Kipindi hicho cha huko nyuma waarabu walikuwa wanakawaida ya kuwapeleka watoto wao vijijini kwa kuwalinda Na mbambo mawili,
Moja, kuwalinda na maradhi ambayo maranyingi yalikuwa yakiwaletea taabu watoto wadogo haswa wakiwa pale mjini makka.
Pili, lengo kubwa pia ilikuwa ni kuwafanya watoto watakao lelewa vijijini wawe Na lafudhi nzuri kabisa ya kuonge lugha ya kiarabu, tofauti kabisa na kiarabu ambacho kinacho ongelewa mijini.
Hivyo Muhammad (s, a, w) hakuchukua muda mrefu Sana akawa amechukuliwa na mlezi mwengine anaeitwa Bi Halimat Saadia.
=====================================
SAFARI YAKE MTUME (s, a, w) MPAKA KIJIJINI.
Baada tu mtume kuzaliwa na Mama yake mzazi Bi Amina bint Wahab, mtume alilelewa katika mikono tofauti tofauti na kwa wakati tofauti tofauti,
Moja ya watu waliomlea na kumnyonyesha mtume muhammad (s, a, w ), malezi bora kabisa alikuwa ni Mama huyu mtukufu Bi Halimat saadiya ambae alikuwa ni mtu wapili kumnyonyesha mtume tena kwa miaka takriban minne (4) ndipo akaamua kumrudisha kwa Mama yake mzazi Bi Aamina bint Wahab,
Kipindi cha huko nyuma waarabu walikuwa na mila na taratibu za kuwapa waarabu waishio vijijini kuwalelea na kuwa nyonyesha watoto wao kwa malipo maalumu watakavyo kubaliana,
SAFARI YA BI HALIMA KUTOKA KIJIJINI
Bi Halimat saadiya akiwa na wanakijiji wengine walifunga Safari ya kutoka huko kijijini na kuelekea mjini kwaajili ya kwenda kutafuta ajira hiyo ya kunyonyesha watoto wachanga wa mjini ili waweze kujipatia ujira kwa kazi hiyo,
Kwa bahati nzuri au mbaya Bi Halima yeye alikuwa akitumia kipando kilicho dhaifu yaani punda wake alikuwa dhaifu Sana kiasi ilimfanya achelewe Sana kifika mjini ktk kutafuta ajira hiya,
Na ilikuwa wanawahi kuanza Safari ya mapema Sana lengo ni kulikwepa jua ambalo lilikuwa kali Sana Na lenye kuleta uchuvu zaidi ktk safari yao hiyo,
Kwakuwa Bi Halima alitumia usafiri dhaifu tofauti na wenzake, ilimsababishia kuchelewa kufika mjini, Na ilikuwa unapowahi kufika mjini yakupasa upite kila nyumba kwaajili ya kutafuta mtoto kwaajili ya ajira hiyo,
Alianza kuingia nyumba ya mzee Abdul Mutwalib babu yake na mtume Muhammad (s, a, w) Na kweli alimkuta mtoto ambae anajika kunyonyeshwa na watu kutoka vijijini,
Walipoanza kuzungumza kuhusu pesa Bi Halima kiukweli aliiona pesa iliyotolewa na mzee Abdul Mutwalib ni ndogo Sana Na ndio ulikuwa uwezo wake Mzee huyu,
Bi Halima akawaomba kwamba ajaribu kupitia nyumba zingine ili kuona pengine atapata mtoto mwenye pesa ya kuridhisha, kwa bahati mbaya Sana Bi Halima kila nyumba aliokuwa akiingia alijibiwa kuwa wamekwisha pita wenzake nawamekwisha wachukuwa watoto,
Basi baada ya kuzunguka Sana Bi Halima bila ya mafanikio ya kupata mtoto ambae atamnyonyesha kwa pesa iliyo nzuri, Bi Halima akaona si vyema kurudi kijijini bure, akaona kwakuwa alichelewa na wenzake wamekwisha muwahi, basi akaona tu si vibaya akamchukue yule mtoto mwenye pesa kidogo,
Subhanallah, Bi Halima aliona maajabu makubwa Sana kwa mtoto huyu ambae ndie mtume Muhammad, s, a, w.
Wakaingia makubaliano ya kumnyonyesha na kumlea kwa miaka miwili kisha amrudishe,
Na lengo kubwa ilikuwa mtoto akilelewa kwenye mazingira ya kijijini huwa anakuwa mwenye afya nzuri Sana, Na anakuwa anakuwa na nguvu nzuri, lakini pia anakuwa anaongea lugha ilinyooka vizuri kabisa,
Lakini pia mtoto anakuwa na akili nzuri Sana tofauti na watoto wanaolelewa mijini,
Bi Halima akambeba mwanae huyo wa ajira na kuanza nae Safari ya kijijini, inasemekana Bi Halima alikuwa pamoja na mumewe kwenye safari hii.
Hapo ndipo Bi Halima alianza kuona miujiza ya mwenye zimungu, Kwanzaa mnyama aliekuwa akimtumia Kama kipando ghafla akawa mwenye nguvu na afya nzuri ya kutembea,
Pili Bi Halima kwakuwa alichelewa kufika mjini bila shaka alitakiwa achelewe na kurudi kijijini lakini chaajabu alipokuwa akirudi aliwakuta wale wenziwe njiani na kuwapita nayeye kuwa mtu wa kwanza kufika kijijini,
Tatu moja ya muujiza aliouona Bi Halima nikuwa jua lilikuwa kali Sana lakini kwake yeye hakuwahi kuliona jua likiwa kali kwani kulikuwa na kiwingu ambacho kiliwafunika Bi Halima na mgeni wake huyo mtukufu toka mwanzo wa Safari ya kutoka mjini mpaka wanafika kijijini,
Hapo Bi Halima kunakitu alikigunduwa kuwa mtoto aliemchukua yeye sio mtoto wa kawaida, na aliendelea kuona miujiza mbali mbali alipo kuwa akimlea kiumbe huyo bora kabisa duniani,
Bi Halima alishangaa kuona maisha ya pale nyumbani kwake yalikuwa yamebadilika Sana kwa kuona mambo yote Yale yaliokuwa magumu yanakuwa mepesi, Kama vile upatikanaji wa Rizki, mazao na mengineyo,
Na chaajabu nikuwa mtoto huyu mtukufu aliyapenda Sana maziwa ya Bi Halima kiasi alikuwa ajitulizana Sana wakati akiyanyonya maziwa Yale,
Baada ya miaka miwili Bi Halima akamrudisha Muhammad nyumbani kwao, huku akilia Sana kwa kurudisha mtoto ambae amekwisha mzoea Sana, lakini pia mtoto mwenyewe pia alimzoea Bi Halima Sana kiasi hakutaka kubebwa na mtu mwingine zaidi ya Bi Halima,
Mzee Abdul Mutwalib alimruhusu kwa mara nyingine Bi Halima akamlee mtoto huyo kwa miaka miwili mingine tena,
Basi Bi Halima alifuhi Sana kumlea mtoto huyu mtukufu,
Miujiza midogo midogo iliendelea mpaka siku ambayo mtume alimtia hofu kubwa Sana Bi Halima na kuamua kurudisha kwa wazee wake,
Siku ambayo mtume alipasuliwa na kusafishwa nyongo na malaika wawili watukufu,
Huyo ndio Bi Halimat saadiya Allah ampe pepo Mama yetu huyu.
Ndugu zangu Mimi binafsi nimeamua kumuadhimisha kuzaliwa mtume kwa staili hii.
Noordin Ally Nshoro
No comments :
Post a Comment