dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, November 24, 2019

Umoja wa Afrika waitolea wito Uingereza kuheshimu maazimio ya Umoja wa Mataifa!

Umoja wa Afrika umeitaka Uingereza kuacha kuvitawala visiwa vya Chagos ambavyo ni sehemu ya Mauritius na kuodoka katika eneo hilo.

Rais wa baraza la Umoja wa Afrika Musa Faki Muhammed ametoa taarifa ya maandishi inayosema kwamba Uingereza inavunja azimio la Umoja wa mataifa kwa kuendelea kuvitawala visiwa vilivopo katika bahari ya Hindi ambavyo ni sehemu ya Mauritius, suala hilo linampa wasiwasi mkubwa.
Muhammed alisema wataendelea kuiunga mkono Mauritius kuhakikisha kwamba eneo hilo linapata uhuru wake kamili, Muda wa miezi sita uliotolewa na Umoja wa Mataifa kwa Uingereza kuondoka eneo hilo umekamilika Novemba 22.

Muhammed aliitaka Uingereza kuheshimu maazimio ya Umoja wa Mataifa na mahakama ya kimataifa pamoja na jumuiya ya kimataifa kuinga mkono Mauritius.

Mahakama ya kimataifa ya haki mnamo Februari 25 iliamua kwamba Uingereza ivikabidhi visiwa vya Chagos kwa Mauritius.

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Mei 22 lilitoa wito kwa uUingeza kuacha kuvitawala visiwa vya Chagos na ikatoa miezi 6 kwa Uingereza kuvikabidhi visiwa hivyo kwa Mauritius.

Kufuatia maamuzi hayo mnamo mwezi Julai, bunge la Mauritius lilichukua uamuzi wa kuweka uongozi wake katika visiwa hivyo.

No comments :

Post a Comment