dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, November 24, 2019

Watu 70 wamepoteza maisha katika mafuriko Kusini mwa Sudan!

Watu sabini wamepoteza maisha katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa Kusini mwa Sudan.
John Abola, Gavana wa mkoa wa Boma kusini mashariki mwa nchi hiyo, amesema kuwa watu 70, wengi wao wakiwa ni watoto na wazee, wamekufa tangu mwezi Oktoba kutokana na mafuriko, na karibu nusu milioni ya raia wanahitaji msaada wa kibinadamu.
Rais Salva Kiir Mayardit alitangaza dharura katika maeneo ya janga mwezi uliopita.

Nchini Sudani Kusini, ambako kumejaa maji kutokana na mvua kubwa tangu Oktoba, watu 800,000 wamepata shida ya njaa na magonjwa.

No comments :

Post a Comment