dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, November 23, 2019

Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu apinga mashtaka dhidi yake!

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ameyakanusha madai ya ufisadi dhidi yake na amesema ataendelea na majukumu yake kama kiongozi licha ya kufunguliwa mashtaka ya rushwa.

Baada ya mwanasheria mkuu wa nchi hiyo, Avichai Mandelblit kumfungulia mashtaka ya kupokea hongo, udanganyifu na kuvunja uaminifu, Netanyahu aliishutumu hatua hiyo na kuyataja kuwa ungo na njama za kisiasa.
Aidha ameitaja hatua hiyo kama jaribio la mapinduzi dhidi ya waziri mkuu. Hatua ya kumfungulia Netanyahu mashitaka imejiri wakati Israel ikikumbwa na mparaganyiko wa kisiasa na inakabiliwa na uwezekano wa kufanyika uchaguzi kwa mara ya tatu ndani ya mwaka mmoja, baada ya Netanyahu na hata aliyekuwa mshindani wake Benny Gantz kushindwa kuunda serikali.

No comments :

Post a Comment