Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, January 10, 2020

MBUNGE WA MALINDI ALLY SALEH AWAHIMIZA WATU WAKE KUJIANDIKISHA!


"Ndugu zangu

Wana Jimbo la Malindi

Kama mnavyojua baadae mwaka huu kutakuwa na Uchaguzi Mkuu mwengine.

Mbali ya kudhibiti viti vyetu vya Ubunge, Uwakilishi na Udiwani, tuna wajibu wa kuchangia kura nyingi za Urais ili mgombea wetu wa Upinzani ashike Dola.

Ni muhimu turudie na tushinde kuliko matokeo ya 2015 ili tupate nguvu ya mara hii kulinda ushindi wetu na 2020 tuunde Serikali kwa kuiondoa CCM.

Lakini ili lengo hilo litimie ni lazima sote kike kwa kiume tutoke kwenda kuchukua vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi ZanID....sote, sote, sote.


Pia zamu yetu ikifika kwenda kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura pia ni lazima tutoke sote, sote, sote.

Tusikubali ujanja, hila au vitisho vya aina yoyote, kutoka kwa yeyote kutuzuia tusipate Vitambulisho vya ZanID na wala kuzuiwa kusajiliwa kwenye Daftari la Wapiga

Jimbo la Malindi tuendelee kuwa mfano bora ili tuchange na majimbo mengine tuweze kuleta mabadiliko 2020

Tunaomba wenzetu wa majimbo yanayotutangulia wahamsike katika hili kwa sababu tumo jahazi moja kuelekea USHINDI 2020.

Ally Saleh
Mbunge
Jimbo la Malindi
Jan 9, 2020."

No comments :

Post a Comment