Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, March 22, 2020

MP ALI SALEH LAMBASTES SMZ ON CORONAVIRUS!

UJUMBE WA WAZI KWA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR ( SMZ) JUU YA MARADHI YA COVID 19 : KUZUIA NDEGE ZOTE ZA NJE ZISIINGIE ZANZIBAR

Assalam aleikum

Sote tunajua kuwa maradhi ya COVID 19 yameingia Zanzibar kama ambavyo yameingia nchi nyingi duniani. Kwa bahati nzuri hata kwetu tumepata kesi chache. Kwetu maradhi hadi sasa hayajaenea, lakini kwa sasa hio sio hoja, maana kuenelea ni suala la fumbo na kufumbua na tunaambiwa yakiingia yakifika mtaaani basi ugumu wa kuyakabili ni mkubwa.

Ninachotaka kusema ni kuwa kwangu mimi, na pengine baadhi yetu hatuoni kuwa hatua madhbuti zinachukuliwa na kama zinachukuliwa ni kwa kuchelewa na pia kama zinachukuliwa hazitoi ujumbe wenye kuonyesha ile urgency inayotakiwa.

Hii ni hatari mno kwa Zanzibar yenye utamaduni wa kukaribiana, utamaduni wa kujali udugu na utamaduni ambao ni wa kukirimiana. Hatua za kuchukuliwa zilipaswa zichukuliwe mapema ili kupunguza uthari lakini hata kwa ajili ya kujenga mazoea.


Ninachoona ni kuwa tunajitayarisha mpaka ugonjwa uingie ndio tuchukue hatua wakati tunaambiwa kila mgonJwa mmoja anaambukiza watu 4 mpaka 6.2 na kwa maana hio kufika watu 1,000 ni suala la hata siku 7 hazifiki.

Sikatai hatua zilizochukuliwa hadi sasa, ubaya ni kuwa kwa hatua hizo bado kumewekwa wazi juu ya watu kuingia tena wakitokea nchi ambazo ugonjwa umetanda na wakija kwa ndege za nje. Tujitayarishe hata kwa ukweli kuwa kunaweza kuwa na kipindi watu kutoka Tanzania Bara watazuiliwa kuingia Zanzibar na kinyume chake, huo ndio ukweli na tuwe tayari nao.

Tangazo la Serikali kuwa imepiga marufuku ndege za kukodi charter planes halitoshi. Tupige marufuku ndege zote  za kigeni kama Qatar, Omar Air na Ethiopian airlines with immediate effect. Zama hizi kuchukua hatua kama hizo ndio uamuzi sahihi.

Kuzuia charter planes ni muhimu sana, lakini any way msimu ulikuwa ndio unakwisha na kwa hivyo kulikuwa na chache ambazo bado zinakuja. Ni kudanganya umma tu, maana hilo ni dogo kufanana na la kuzuia ndege zenye scheduled programs.

 Sisi tusifanane maamuzi yetu na Serikali ya Muungano, maamuzi yetu yawe yetu, maana sisi ni kisiwa na sisi iwe ni sisi. Tuzuie ndege za kigeni ambazo hata hivi leo zimeingia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar. Sisi tusiweke watalii mbele wala tusiweke kodi za viwanja ya ndege zinatua kujitia kwenye janga.

Eti kuuambia umma kuwa atakayekuja akifika atawekwa QUARANTINE kwa gharama yake mwenyewe, what a heck is this. Kwa nini atengezewe mazingira ya kuja? Zuia ndege zote na utakuwa huna headache ya kukusanya watu, kuwabeba, kuwawekea ulinzi na kuwatia hatarini hao watakaohudumia walioko kwenye self quarantine.

Nimesema hapo juu hatua zinazochukuliwa hazichukuliwi kwa muda unaotakiwa maana hata kwa mgonjwa wetu wa kwanza halikuwa kama la dharura, hali kadhalika wa pili. Hata utoaji wa taarifa umekuwa ukidorora mpaka baadhi ya watu wasukume sukume.

Hakuaonekani kuwa na centralized position ya kutoa taarifa. Wa Afya, wa Makamo wa Pili, wa Utalii. Kipindi hiki Waziri wa Afya inatakiwa azuiliwe likizo na kazi yake kuu kwa sasa iwe ni jambo hili, maana likiripuka itakuwa ni janga.  Hio pia kwa mawaziri wote wanatakiwa wawe katika hali ya dharura, maana maradhi ya mripuko ni suala mtambuka, kama yalivyo maamuzi na hatua zake.

Lakini pia inaelekea hakuna maamuzi yanayoweza kufanywa kwa approach inayofanana na dharura hii yaani drastic na draconian. Sijui kuna maslahi gani ya kuziachia hizo ndege ziendelee kuja hapa Zanzibar ilhali madhara yake yanajulikana.

Hivi wenzetu hasa mataifa makubwa yenye uwezo kama Marekani, Uingereza hata nchi nyengine kama India, Pakistan nazo zimezuia ndege, sisi ni nani ambao hata vyumba vya dharura 10 hatuna, au hata hayo mahema yaliojengwa sijui kama yanaweza kuhudumia watu 100 kwa wakati mmoja.
SMZ  ndio masu-ul  na ina wajibu wa ku take leadership position. Hili la ndege za nje lifanyiwe maamuzi roho zetu zitutue. Mtabeba jukumu kubwa leo na kesho kiama.

Mtakuwaje ugonjwa ukienea na umma ukiteketea?

Kukuthibitishia kuwa hakuna umakini stahiki katika ngazi ya Serikali tazama video za Bw Mahmoud Thabit Kombo alivyokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Kwa sasa jambo kubwa duniani na hatua muhimu ya kuzuia maradhi ni social-distancing, na hii iwe zaidi ya mita 100 baina ya mtu na mtu. Hilo halikuzingatiwa kabisa na hio inaonyesha ndio hali halisi ya kiwango cha awareness au kujali kwetu.

Haielekei kuwa watu wana enforce hili la social-distancing sehemu kadhaa kwa sababu tu tunadhani mtaani hakuna mgonjwa kwa sababu hajafika hospitali na kwa sababu Serikali haijatangaza, ambapo tunajua pia kuna enforcement isio madhubuti kwa watu ambao hawaingia Unguja au Pemba kwa viwanja au bandari rasmi.

Mawazo yangu ni kuwa lazima tuanze kuwajenga watu wetu kwa njia ya kuwabadilisha tabia ili pakitokea mripuko kuwa kuna uelewa. Kitatugharimu sana kungoja mripuko ndio tuanze kufukuzana na wananchi wafanye hiki au wafanye kile.
Najua kuna wataalamu, najua kuna mkakati lakini mkakati mkubwa na kuzuia uingiaji wa wageni ambao ndio chanzo kikubwa cha kuingiza ugonjwa ndani ya nchi. Natumai SMZ mtalipa uzito hili.

Ally Saleh Alberto
Mbunge wa Malindi
March 21, 2020

No comments :

Post a Comment