zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, July 8, 2020

NANI KAMA MAMA???....A real picture of a Mother's Love!

Picha hii ilipigwa mwaka 2013 katika mbuga ya wanyama ya Maasai Mara, nchini Kenya na mpiga picha za wanyama (wildlife photographer) Alison Buttigieg, na ilishinda kuwa picha bora ya mwaka katika tuzo za habari huko Australia.

Swala huyu anayesulubiwa na chui hawa, ni Mama wa watoto wawili. Akiwa na wanawe kwenye maskani yao, walivamiwa na chui waliokuwa na njaa. Watoto wake walikuwa wadogo na hawakua na nguvu za kuweza kukimbia na kujiokoa. Mama yao angaweza kuaamua kukimbia na kuwaacha wanae ambao wangeweza kuwa chakula cha chui.


Lakini hakuwaacha alikimbia nao. Baada ya umbali kidogo akaona chui wamemkaribia. Akaacha wanawe waende na yeye akapunguza mwendo. Alitaka kuhakikisha wanawe wanakuwa salama hata kama yeye atadhurika. Chui wakamfikia na kumparamia.

Katikati ya chui wawili bado aliweza kusimama wima na kuwatazama wanawe ambao walikuwa wakizidi kuyoyoma porini. Alikuwa akiwatizama kwa mara ya mwisho maana alijua hatawaona tena!!! Ilikuwa ishara ya kuwaaga.

Kwa macho yenye ujasiri aliwaaga wanawe. Aliwakodolea macho hadi wakapotelea kabisa porini kabla ya kukubali chui kumgeuza chakula. Alihakikisha kitu cha mwisho kuona kwenye macho yake ni taswira ya wanawe.

Ilikuwa ni ishara ya kuwaaga. Alijua hatawaona tena, lakini hakusikitika maana alijua kifo chake kilikua ukombozi kwa wanae.

Picha hii inatuonyesha taswira halisi ya Upendo wa Mama....picha hii ni maalum kwa wanawake wote..msiogope..Mungu yuko nanyi..pambaneni.waleeni watoto wenu kwa misingi na maadili mema.

No comments :

Post a Comment