dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, September 23, 2020

WANACHAMA, VIONGOZI 28 WA ACT-WAZALENDO ZANZIBAR MBARONI PEMBA!

VIONGOZI na wanachama 28 wa Chama cha ACT-Wazalendo Mkoa wa Kaskazini Pemba, Zanzibar wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujeruhi na kuwafanyia fujo wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatano tarehe 23 Septemba 2020 na, Juma Sadi Khamis, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati akizungumza na MwanaHALISI Online. 

Kamanda Khamis amesema, watu sita walikamatwa kwa tuhuma za kuchora nyuma za wanachama wa CCM huku 22 wakikamatwa kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kujeruhi wanachama watatu wa CCM katika Msikiti wa Kandagani visiwani humo.
“Kulikuwa na matukio ya kuchorwa baadhi ya majumba yanayolengwa ya CCM, baada ya kupata taarifa hiyo, tulifanya operesheni kuanza kuwatafuta wanaohusika, tuliwakamata watu sita na tunaendelea nao na utaratibu wa kesi,” amesema Kamanda Khamis. 

Kamanda Khamis amesema “baada ya hilo, ikatokea tukio la kushambuliwa msikiti na kupigwa wanachama wa CCM tukio limetokea alfajiri ya jana Jumanne tarehe 22 Septemba 2020, tumeanza opereshehni na watu 22 tumewashikilia.” 

Kamanda Khamis amesema, Jeshi la Polisi linaendelea kuwashikilia watuhumiwa hao kwa ajili ya uchunguzi zaidi. 

“Tunahoji baadhi ya viongozi wa wilaya wa ACT, tunawahoji kwa nini wanachama wenu wanafanya fujo wanaingia msikitini kushambulia, tuaendelea na upelelezi kwa yeyote anahisi kuna jambo limetokea ni vyema kuripoti sisi jukumu letu ni kulinda usalama wa raia,” amesema Kamanda Khamis ambaye hakuwa tayari kuwataja majina yao 

Kuhusu hali za wanachama watatu wa CCM waliojeruhiwa msikitini, Kamanda Khamis amesema, mmoja ameruhusiwa kurudi nyumbani huku wawili wakiendelea na matibabu katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Mjini Magharibi Unguja. 

“Waliojeruhiwa vibaya ni wawili, taarifa mwanzo ni watatu lakini mmoja ameruhusiwa aliparazwa na panga, mmoja alikatwa sehemu ya koo mmoja amemumia mkono, wawili hao hospitali wamehamishiwa Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Magharibi,” amesema Kamanda Khamis. 

Kamanda huyo wa Polisi Kaskazini Pemba amewaonya wanasiasa na wafuasi wao kuacha kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani katika kipindi cha kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020. 

Kamanda Khamis amesema atakayejaribu kujihusisha na vitendo hivyo atapambana na Jeshi la Polisi. 

“Hiki kipindi cha kampeni tunakwenda katika uchaguzi, wananchi kwa ujumla wanaojihusisha na uhalifu dhidi ya masuala ya siasa waache mara moja na yeyote atakayekiuka maagizo haya sheria zipo, yoyote atakayejaribu kuharibu amani tutapambana nae,” ameonya Kamanda Khamis.


No comments :

Post a Comment