Maalim Seif - Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya GNU ya Zanzibar.
Aandika Maalim Seif Sharif Hamad:
"Wa Alaykum Salaam.
Naomba kuwajulisha kuwa Jumatatu niliomba nipimwe Covid 19 mimi na mama yenu baada ya kupata nimonia kali. Jumanne tukapimwa. Rapid test ilionesha viashiria kwa kuwepo kwa covid 19. Nikashauriwa mimi na Bi Aweinah tuji- self isolate tukianza kupata madawa.
Test halisi leo zimethibitisha kuwa tunayo. Baadhi ya walinzi wangu 3, Hassan na Alii na Mayasa wameonekana na viashiria kwa rapid rest. Baada ya saa 72 ndio watapata confirmation.
Leo nimepata matatizo ya kupumua. Hivyo mnamo saa 11.45 jioni nimelazwa Mnazi Mmoja kwa close supervision.
Madaktari wamejitahidi sana. Sasa sijambo na matibabu yanaendelea.
Bibi Aweinah hajambo. Yuko self-isolation nyumbani.
Musiwe na wasi wasi. Zidisheni dua tu. Mungu Ataninyanyua, Amin".
No comments :
Post a Comment