dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, October 27, 2021

SHAIRI: FATUMA KATUANGUSHA, KATUVUNJIA HARUSI!

48 HOURS BAADA YA KUFIKA MUSCAT,  RAFIKI WA KIJANA ALIEOA UNGUJA AFIKA HOTELINI KUMUONA BABU WA FATUMA !

Hongera na nyingi pole, kwa safari yako ndefu,
Umeruka toka Dole, mpaka kwetu Galfu,
Umeacha yako tele, wewe kweli ni sharifu,
Fatuma katuangusha, katuvunjia harusi.

Pili shikamoo zangu, tafadhali zipokee,
Maskati mji wangu, tutoke tukatembee,
Ukawaone wenzangu, vijana pia wazee,
Fatuma katuangusha, katuvunjia harusi.

Mimi soyule kijana, Unguja alieoa,
Bali rafikie sana, jina langu nitatoa, 
Yeye kaondoka jana, kaelekea Samoa,
Fatuma katuangusha, katuvunjia harusi.

Hakuwa nayo habari, Maskati utashuka,
Angelivunja safari, kiwanjani angefika,
Ingelikuwa vizuri, kama mngekutanika,
Fatuma katuangusha, katuvunjia harusi.

Kabla kitu chochote, na tukale cha usiku,
Halafu nikupe yote, yalojiri ile siku,
Katuelezea sote, alipowasili huku,
Fatuma katuangusha, katuvunjia harusi.

Wala hajakasirika, kwa mahari bilioni,
Kwa pesa za Afrika, huku kwetu rialeni,
Alikereka hakika, baada kuingia ndani,
Fatuma katuangusha, katuvunjia harusi.

Alikereka hakika, baada kuingia ndani,
Tano kupita dakika, chozi latoka machoni,
Ilikuwa heka heka, hasa pale mlangoni,
Fatuma katuangusha, katuvunjia harusi.

Huku akihangaika, kakimbilia garini,
Baada jua kutweka, yeye atua Omani,
Harusi ilivunjika, ulijua ni kwanini???
Fatuma katuangusha, katuvunjia harusi.

Kwa ufupi ya swahibu, harusi haikujibu,
Kwetu sisi waghaibu, hii ni kubwa aibu,
Na kweli ndio sababu, mambo ilo yaharibu,
Fatuma katuangusha, katuvunjia harusi.

Na vipi wako mgeni, akaribishwa makombo?
Si ungelitiwa ndani, siku za Thabiti Kombo,
M-baya utamaduni, wakunukishana shombo,
Fatuma katuangusha, katuvunjia harusi.

Ni Habibu na Shaibu, wote wanapokezana,
Wanahitaji tabibu, tena haraka sana, 
Nini kina waghilibu, hii sasa ni laana,
Fatuma katuangusha, katuvunjia harusi.

Fatuma yake maringo, aendesha gari tupu,
Labda we  ni utingo, haukuwashi upupu,
Au unatoka Kongo, na hujui kunywa supu?
Fatuma katuangusha, katuvunjia harusi.

Tamati narudi nyuma, nakumbusha taratibu,
Umuulize Fatuma, ili upate majibu, 
Nani hasa mhujuma, Habibu au Shaibu?
Fatuma katuangusha, katuvunjia harusi.

/Muscat, October 27, 2021.

No comments :

Post a Comment