Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, October 16, 2021

ZACADIA YATOA UJUMBE WA HARAKA KWA WANACHAMA WAKE!


ZACADIA ambayo ni moja kati ya Jumuiya za Wazanzibar wanaoishi Canada (Zanzibar-Canadian Diaspora Association) yenye makao makuu yake jijini Toronto, imewasambazia Wana-Jumuiya wake kupitia emails na WhatsApp ujumbe wa haraka.

Ujumbe huo ulianza hivi:

"
Wanachama Wetu Wote,
Baada ya yale yaliotokea kule Leicester (UK) tumepigiwa simu na baadhi ya wanachama wetu wakitaka kujua usalama wa michango yao katika Jumuiya yetu ya ZACADIA.

Kama Mshika Fedha Mkuu (Chief Treasurer) na Vice-President wa Jumuiya, nachukuwa nafasi hii kuwahakikishia na kuwajulisha wote kuwa michango yenu ni salama na imo katika mikono madhubuti na yenye kuaminika. 

Japokuwa bado hatujayajua vizuri yaliotokea huko Leicester, lakini mambo kama hayo hayatotokea kwenye Jumuiya yetu, kwasababu ya vithibiti vifuatavyo tulivyoviweka ili kulinda michango yenu mikononi mwetu:
[1] Pesa zote za michango zipo benki na kutoa hata Dollar 
       moja benki kwaajili ya shughuli za Jumuiya ni lazima 
       Board Members watatu wanaotambulika na benki waende 
       benki kutaka hizo pesa. 
[2] Hao Board Members watatu ni lazima waende benki 
       physically na wa-apply kutaka kutoa hizo pesa.
[3] Hatuna mpango wa checque book na kwahivyo mtu akiiga 
       signatures za Wana-Bodi ni kazi bure.
[4] Account ipo online, lakini hakuna hata mtu mmoja 
       anaeweza kutoa pesa online na kuzipeleka pahala pengine.
[5] Tunazo bank cards, lakini ni za kuulizia balance tu na 
       huwezi kuzitumia kwenye ATM kutoa pesa au kununulia 
       kitu dukani.

Mwanzo tuliona tumejiwekea masharti magumu ambayo wakati mwengine sisi wenyewe yanatupunguzia kasi ya kufanya haraka haraka kazi zetu za Jumuiya, lakini baada ya haya tunayoyasikia yametokea huko Leicester, tunahisi kuwa kumbe tupo kwenye mstari ulionyoka na kwahivyo wanachama wetu msiwe na wasiwasi hata kidogo juu ya michango yenu mnayotoa.

Zaidi ya yoyote ni kuwa mtu yoyote yule ambae aliwahi kutuchangia,  basi mtu huyo anayo haki yakutaka statement of accounts ya mwaka wowote ule ili kuona matumizi yalikuwa vipi na kiasi gani ilikuwa balance mwisho wa mwaka huo. 

Ukitaka kupokea statement of accounts, basi peleka email to < communications@zacadia.com> na kwenye subject weka Statement of accounts 2017, kama unataka statement ya mwaka 2017. Kama unataka ya 2020 basi weka kwenye subject Statement of accounts 2020.

Hatupendelei kuzitoa statements za mwaka kwenye ma-blogs ili watu wote waone, japokuwa kwa kuweka hesabu zetu wazi tungelipendelea kufanya hivyo. Lakini, tunaogopa scammers wasione account imenona wakaanza kutuandama na kwahivyo statements of accounts tunatoa individually kwa yule anaetaka tu. Kama mtu hajatosheka na yale yaliomo kwenye statement of accounts anaweza kumuona Chief Treasurer kwa maelezo zaidi.

Kwa haya maelezo mafupi tunadhani tumeweza kukutoweni shaka wanachama wetu na kuwa michango yenu ipo salama.

Tunapenda pia kuchukuwa fursa hii kuwajulisha wote kuwa mwisho wa mwezi huu wa October 29th, 2021, tutapeleka tena Zanzibar vitanda vya hospitali kama 75 na wheelchairs 25 - kama tulivyofanya mwaka jana


na kwahivyo tunaomba kila anaetaka kutabaruku kutumia njia zetu zile zile za kutuma michango ambazo ni:

[1] By email: < treasurer.zacadia@gmail.com>

[2] Direct to our bank account: 
      Bank of Montreal (BMO)
      Account #8977-348
      Institution #001
      Branch transit #03732

Kila la kheri".



No comments :

Post a Comment