Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, January 12, 2022

ZANZIBARNIKWETU PRESENTS TO YOU OUR NEXT SPEAKER!

NI NANI ANDREW JOHN CHENGE ?

Kalamu ya Mwl. Udadis

KUZALIWA

- Mbobezi wa Sheria Barani Afrika na "Alumni" wa Chuo kikuu bora Duniani- Havard cha Nchini Marekani Mh.Andrew John Chenge alizaliwa mwaka 1947 nchini Tanzania (Tanganyika wakati huo).

ELIMU

- Nguli huyu wa Sheria alianza safari ya kitaaluma katika Shule ya msingi Sasago (Musoma) kati ya mwaka 1955- 1958

- Kisha akajiunga na St. Pius Seminary Makoko Musoma kati ya mwaka 1959-1962

- Kisha akajiunga na St.Mary's Seminary Nyegezi mwanza kati ya mwaka 1963-1966 kwaajili ya masomo ya Sekondari.

- Kati ya mwaka 1967 - 1968 alijiunga na Mkwawa High school.

- Mwaka 1969 alikuwa kati ya wanafunzi wachache waliojiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwaajili ya masomo ya Sheria (LL.B) na kufanikiwa kuhitimu kwa ufaulu wa juu mwaka 1972.

- Mwaka 1974 - 1975 alibahatika kuwa kati ya wanasheria wachache Duniani kujiunga na Chuo Kikuu cha Havard kwaajili ya Shahada ya uzamili aliyohitimu kwa ufaulu mkubwa.

UTUMISHI NA UZOEFU SERIKALINI


- Kati ya mwaka 1972 - 1990 alihudumu kama mwanasheria wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

- Kati ya mwaka 1990- 1992 alihudumu kama Naibu Mwanasheria Mkuu (D/AG)

- Kati ya mwaka 1993 -2005 alihudumu kama Mwanasheria mkuu wa serikali.

- Mwaka 2006 alihudumu kama Waziri wa Kwanza wa Ushirikiano wa Afrika mashariki

- Kati ya 2006-2008 alihudumu kama Waziri wa miundombinu katika serikali ya awamu ya nne.

UZOEFU KATIKA BUNGE

- Kati ya mwaka 2005 - 2020 alihudumu kama Mbunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi

- Kati ya mwaka 2008 - 2010 alihudumu kama mjumbe wa kamati ya Bunge ya Uchumi na Fedha.

- Kati ya mwaka 2012-2013 alihudumu kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi na Fedha

- Kati ya mwaka 2013-2015 alihudumu kama Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Bajeti

-Kati ya mwaka 2015- 2020 alihudumu kama Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Sheria na pia kama mmoja wa Wenyeviti 3 wa Bunge.

No comments :

Post a Comment