"Tupo tayari na maandalizi yote tushayamaliza", alielezea bi Shahida alipohojiwa na blog hili kuhusu usiku huu maalumu wa akina mama wa ki-Zanzibari wa Toronto.
"Nia ni akina mama kukutana pamoja na kubadilishana fikra na mawazo juu ya mambo mengi yanayoendelea duniani hivi sasa na katika maisha yetu", aliendelea bi Shahida Hamad ambae ndio kinara wa Management Team ya Zacadia ambayo imeudhamini usiku huu.
Zacadia ni moja katika Jumuiya za Wazanzibari wanaoishi nchini Canada ambayo makao makuu yake yapo mjini Toronto.
Tokea Summer ya 2022 kuanza, Zacadia imekuwa mstari wa mbele katika juhudi za kuwakusanya Wazanzibari pamoja na shughuli yao itakayofuata baada ya hii ya leo kumalizika itakuwa ni picnic itakayofanyika tarehe 13 August kwenye ile Park inayopendwa sana na watoto katika jiji la Toronto iitwayo Earl Bales Park ambayo ipo kwenye barabara ya Bathurst nambari 4169.


No comments :
Post a Comment