dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, September 25, 2022

TANZANIANS ABROAD ARE UNITING TO FIGHT FOR THEIR INALIENABLE RIGHT!


Watanzania wenye uraia wa nchi za nje wamekusanyika pamoja kwenye WhatsApp group linalojulikana kwa jina la TANZANIANS FOR DUAL CITIZENSHIP.

Group hili lilianzishwa mnamo tarehe 4 mwezi huu wa tisa kwa niaba ya wote wale waliozaliwa Tanzania na sasa wameupoteza uraia wao huo wa kuzaliwa kutokana na kuchukuwa uraia wa nchi nyengine.

Tayari zaidi ya Wana-Diaspora 500 washajiunga kutoka takriban nchi zote za duniani na inategemewa baada ya muda mfupi maelefu watakuwa washajiunga na group hili. 

Kujiunga pamoja kwa kasi hii kubwa kwa Wana-Diaspora wa Tz kwenye hili group inaonesha wazi hamu ya Watanzania kuwa na uraia pacha.

Group linaeleza nia yake kama..."Nia ya Group hili ni kuunganisha nguvu ya watanzania ktk umoja wetu ktk kudai Uraia Pacha bila kujali vyama vya siasa, kanda, wala ubaguzi wa aina yeyote ile. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu."

Mmoja katika wanaharakati aliandika huko nyuma  kuwa..."IELEWEKE KUWA, LENGO LA GROUP HILI NI MOJA TU, KUPELEKA KESI MAHAKAMANI KUUDAI URAIA WETU WA TANZANIA. Mengine yote yatajadiliwa kutokana na matokeo ya kesi yetu ya msingi......"


Mwanaharakati mwengine aliandika ...."Hili group ni specifically kwa wanao-support dual Citizenship only, if you are not, you are in a wrong group. Lengo ni kuwaunganisha wote wanounga mkono uraia pacha kuona number ya watanzania walio serious ili tuje na serious campaign ya hili suala linalopigwa dana dana muda mrefu".

Wengi ya Wana-Diaspora inaonesha wamefurahi kuundwa kwa hili group ili wapate kupaza sauti zao na vilio vyao kuhusu uraia pacha. Zaidi ya msgs elfu moja zinakuwa exchanged kila siku ukumbini. 

Mwana-ukumbi mmoja kaonesha furaha yake kwa kuandika..."Leo ni siku nzuri sana kwa diaspora kuanza na deal na mambo yanayowahusu.
This is our major project ever to all Tanzanian diasporas and coming foreign born Tanzanian kids anywhere they may be plus aspirant coming Tanzanian generations who may migrate elsewhere in this planet for jobs or education business or anything.
Protection of their birthright and country of origin
We are in this together until we win all." 


Wanaojiunga kwenye hili group sio Wana-Diaspora tu bali pia hata Watanzania wa nyumbani wanaoukubali urai pacha. 

Aandika mmoja kutoka county ya Texas (Marekani)....
"Let’s be positive 
Labda hawajui 
Labda waoga 
Labda hata hawajui kuwa kuna watoto wa mtanzania wa kawaida ameweza kuishi na kufanya kazi uk , Germany , Sweden , USA, Japan etc 
We need to engage on educating everyone who we are why we need to stay Tanzanian.
Kila mmoja humu awe balozi 
Tunakwenda mahakamani pamoja na mambo mengine to bring awareness Ndani ya nchi yetu Nani ni diaspora 
Nani wanataka haki ya kuzaliwa 
Nani wanataka dual citizenship 
We have to bring this conversation back home and to all diasporas around the world
Umoja wetu ushindi wetu"

Tayari Tshirts zenye logo hio hapo juu zinauzwa kwa Dollar 20 tu, ili kuusambaza ujumbe na msimamo wa Wana-Diaspora hawa kuhusu uraia pacha.

Ili nia yao hii ya kuipeleka serikali mahakamani ifuzu, watahitaji kukusanya  sio chini ya Dollar za kimarekani kama 50,000 ambazo hazionekani kuwa ni kikwazo kwao, kwani  zaidi ya Watz milioni moja wanaishi nje.

Well, kama hili group kweli lina-mean business basi tunalipa HEKO na tunaliunga mkono MIA kwa MIA, kwasababu haifahamiki iweje mtu aporwe haki yake ya kuzaliwa kwa kuchukuwa pasi nyengine ya kusafiria? Wengi wanachukuwa uraia wa nje out of necessity and not out of convenience!

Upo uwezekano wa hili group kutokushinda kesi yao, lakini ujumbe utakuwa umeshafika serikalini na kwahivyo hakuna kuvunjika moyo bali ni kusonga mbele tu!

Kama desturi yetu Wana-Bongo, kwa lolote lile ni lazima tupingane hata kwa lile jambo lenye manufaa mapana kwa sote. Hivyo basi limezuka group jengine la WhatsApp ambalo hilo linapigania Hadhi Maalumu. But, the question is: Why going for silver when you can go for gold?  - Of course hawa watakuwa wale ambao kama ikikubaliwa Dual Citizenship wao au jamaa zao hawato-qualify. Kwahivyo, kwao ni bora kupata chochote kuliko kukosa yote!

Frankly speaking, if you get down to the nitty-gritty of this issue, bora serikali kwa mapema ikubali maoni ya wengi kuliko kungojea kupelekwa mahakamani na wazawa, kwasababu huko mbele Tanzania haitoweza kuzuwia wimbi la wengi wanaotaka uraia pacha. 

Hadhi Maalumu sounds good, but not to WAZAWA!
Let's give Special Status to those who do not qualify for our Dual Citizenship requirements!

CAUTION: Any opinion expressed in this blog does not necessarily reflect the view of the blog's owner.


No comments :

Post a Comment