zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, September 19, 2022

ZACADIA KUANZA PROGRAMS MPYA KATIKA MSIMU WA BARIDI!

Baada ya kumaliza msimu wa joto (Summer) kwa picnic yao ya jana iliyofana, ZACADIA inataka kuanza msimu wa baridi unaokuja kwa kuwakutanisha tena akina mama wa Toronto na vitongoji vyake kwenye usiku ambao umebatizwa jina la LADIES' NIGHT!

"Tulifanya huko nyuma LADIES' NIGHT, kwavile ilikuwa ni mara ya mwanzo tulitegemea mahudhurio kuwa madogo, lakini waliohudhuria walikuwa zaidi ya mara tatu ya idadi tulioifikiria mwanzo na kwahivyo sehemu ilikuwa haikutosha kwa akina mama kujitanua na kwavile tulikwa wengi joto lilituandama", alielezea bi Shahida Hamad anaejulikana mjini Toronto kwa jina la umaarufu kama Da Shaa na ambae ndio Team Leader wa Management Team ya Zacadia.

"Kwahivyo safari hii tunataka kuwalipa akina mama kwa kuwakusanya pahala pakubwa na pazuri zaidi. Tunakusudia kukutana hotelini au sehemu kubwa yoyote ile panapofanyiwa sherehe za harusi", aliendelea bi Shahida au Da Shaa kulielezea blog hili.

"Ni muhimu kwa sisi akina mama kukutana na kubadilishana mawazo bila ya muda mrefu kupita, ili tupate kuwa pamoja zaidi. Hii ndio nia yetu. Tunaanza na hii Ladies Night katika huu msimu wa baridi unaokuja na baadae tutaendelea na programs nyengine tele ambazo tayari zipo jikoni", alielezea Da Shaa.

"Kwahivyo, tunawataka akina mama wote wa Toronto na vitongoji vyake wakae mkao wa kula (stay tuned). Tupo mbioni kuandaa huu usiku wetu maalumu wa akina mama ili tupate kujimwaga na kubadilishana fikra juu ya mengi yanayoendelea leo nyumbani na duniani", alimalizia Da Shaa.

Zacadia ni moja katika Jumuiya za Wazanzibari wanaoishi Canada. Makao makuu ya Jumuiya hii ni mjini Toronto. Jumuiya hii ni kama kiungo baina ya watu wenye asili ya Zanzibar wanaoishi Canada na wale Wazanzibari wa Visiwani.

No comments :

Post a Comment