Tanzania Diaspora in Oman (TADIO) ikishirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Oman imemualika Rais wa Zanzibar Dr. Hussein Mwinyi katika mkutano utakaofanyika tarehe 12-October - 2022.
Hii inakuja wakati vita kali inaendelea online baina ya WaTz wanaoishi ughaibuni wanaotaka Uraia Pacha na wale wanaotaka Hadhi Maalumu.
Serikali ya Tz tayari ishatamka tokea huko nyuma kuwa inaifanyia kazi Hadhi Maalumu, lakini mpaka leo bado hili suala halijamalizwa, ikipelekea WaTz wengine kupata tamaa kwamba wanaweza kuishawishi serikali kubadilisha mtazamo wake juu ya jambo hili kupitia mahakama.
Zanzibar tayari ishaipokea Hadhi Maalumu na haijulikani kwenye mkutano huu kama hii ishu itatajwa au vipi.
Kwavile hii Jumuiya ni ya WaTz wote na sio WaZnz tu, wengi wanakubali kuwa huenda ishu hii ikazungumzwa kirefu hasa kwavile watu wengi wenye asili ya Tz wanaishi Oman hivi sasa.

No comments :
Post a Comment