Sisi Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi, CCM (UWT) tumepokea kwa furaha kubwa kitendo cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kumtunuku Shahada ya Udaktari wa Heshima Rais na Mwenyekiti wa Chama chetu cha Mapinduzi, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.
Umoja wetu wa UWT tunampongeza Dkt Samia tukitambua juhudi zake zisizomithilika za kuleta maendeleo maridhawa nchini katika muda mfupi wa miaka miwili Ikulu.
Mwenyekiti wetu Dkt Samia, kama ambavyo amekuja na Falsafa yake ya (4R) ya uongozi bora; Reconciliation (Maridhiano), Resiliency (Ustahamilivu), Reforms (Mabadiliko) na Rebuilding (Kujenga Upya), ameleta Mapinduzi makubwa katika kila Sekta nchini na hivyo anastahili kupongezwa.
Ni dhahiri sasa kupitia falsafa hii ameirejesha Nchi katika uimara wake kiuchumi, kisiasa na kijamii tukizingatia ameipokea Nchi yetu katika wakati mgumu wa kuondokewa ghafla na Mtangulizi wake Rais Magufuli, gonjwa la Corona na Vita ya Urusi na Ukraine
No comments :
Post a Comment