Baada ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuruhusu Wana-Diaspora wa Tanzania kufungua akaunti katika benki za nyumbani, Wana-Diaspora wengi wameonesha hamu kubwa mpaka kufikia hatua ya kufungua grupu ambalo linazungumzia habari za benki za nyumbani tu na vipi wanaweza kufaidika na huduma za nyumbani za kibenki.
Ili kupata maelezo zaidi, blog hili lilimtafuta kwa njia ya simu Ndugu Hassan Othman wa Toronto (Canada) ambae ni veteran wa low fees remittances to Africa na ambae ndie alieipeleka WorldRemit kutoka Canada kuenda Tanzania akishirikiana na benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ Ltd) katika mwaka 2012 na ni mmoja wa Admin wa hili grupu.
Kwanza, tulianza kwa kumuuliza Ndugu Othman nini ilikuwa nia ya grupu hili, nae alitujibu kama ifuatavyo:
"Nia yetu kubwa ni kujuvyana juu ya fursa mbali mbali Wana-Diaspora wanaweza kuzipata kupitia benki za nyumbani kwetu".
Aliendelea..."Ukiwa nje na ukiwa upo kwenye benki fulani nyumbani, basi unaweza ukapata mikopo ya nyumba (mortgages), loans kwa miradi yako binafsi kwa riba nafuu, bima ya maisha, bima ya afya, etc. etc. In fact, yote yale ambayo tunayapata huku ughaibuni unaweza ukayapata nyumbani pia, japokuwa sio to the same level kama huku nje. Inategemea uhusiano wako na benki yako ya nyumbani na vipi una-negotiate nao. Nia ya grupu hili ni kupeleka ujumbe huu kwa wenzetu wote wanaoishi huku nje, kwani sio wengi wanaojua juu ya hizi habari nzuri za nyumbani za hivi karibuni kutoka BoT".
"Pia, kwenye grupu wapo wawakilishi ambao ni wataalamu wa benki tafauti na kwahivyo ni uwanja wa kuuliza masuala yoyote yale ya kibenki na wataalamu watakujibu au kukuongoza inavyofaa. Kila mtaalamu anajibu masuala yanayohusu benki yake na sio kuhusu benki ya mtaalamu mwengine. Kabla mtaalamu hajajibu inabidi ajitambulishe yeye ni kutoka benki gani. Kwahivyo, hapana upotoshaji au ubabaishaji wa aina yoyote ile. Mtaalamu analolisema kwenye grupu ni msimamo wa hio benki yake anayoiwakilisha".
Blog liliendelea na kumuuliza Shk Othman, ni wawakilishi au wataalamu wa benki gani ziliopo kwenye hili grupu mpaka hivi sasa?
Yeye alijibu kuwa,.."Inafurahisha kuwa tumeanza hizi harakati juzi juzi tu, lakini benki nyingi za nyumbani zimetuunga mkono na kwa sasa kwenye hili grupu wapo wawakilishi wa benki zifuatazo:
AMANA BANK
AZANIA BANK
CRDB BANK
EQUITY BANK
EXIM BANK
NMB BANK
STANBIC BANK".
Aliendelea Nd. Othman,..." Benki kubwa ya kule Zanzibar ijulikanayo kama The People's Bank of Zanzibar - (PBZ Ltd) ambayo ni Chaguo la wengi kule nyumbani, pia imeonesha nia na hamu ya kumuweka mtaalamu wake kwenye hili grupu, kwani Wana-Diaspora wengi wanaulizia juu ya vipi wanaweza kufungua akaunti au kufaidika na huduma tele tele wanazozitoa benki hii kule Visiwani".
Blog pia lilitaka kujua kutoka kwa Ndugu Othman kuwa vipi kwenye grupu lao wanadhibiti migongano ya fikra kwa hizi siku za siasa za uwazi?
AMANA BANK
AZANIA BANK
CRDB BANK
EQUITY BANK
EXIM BANK
NMB BANK
STANBIC BANK".
Aliendelea Nd. Othman,..." Benki kubwa ya kule Zanzibar ijulikanayo kama The People's Bank of Zanzibar - (PBZ Ltd) ambayo ni Chaguo la wengi kule nyumbani, pia imeonesha nia na hamu ya kumuweka mtaalamu wake kwenye hili grupu, kwani Wana-Diaspora wengi wanaulizia juu ya vipi wanaweza kufungua akaunti au kufaidika na huduma tele tele wanazozitoa benki hii kule Visiwani".
Blog pia lilitaka kujua kutoka kwa Ndugu Othman kuwa vipi kwenye grupu lao wanadhibiti migongano ya fikra kwa hizi siku za siasa za uwazi?
Nae alitujibu kuwa... " Tunayo miongozo yetu inayotuongoza. Sisi hatupo pale kwaajili ya mijadala ya mambo ya siasa. Kwanza kabisa hairuhusiwi ku-post kitu chochote kisichohusu mambo ya kibenki. Lakini, kama unavyojua ndugu muandishi kuwa, it is very difficult to control a human being, kwani juu ya kukataza kwetu kote, still baadhi ya wakati wengine wana-post wanayoyapenda wao. Kwa bahati nzuri, tumebahatika kuwa na ma-Admin mahodari na wakali, kwani uki-post upuuzi wowote ule basi posting yako inakuwa deleted hapo hapo na wale wabishiwabishi huwa wanatolewa kabisa kutoka kwenye grupu. Ni hatua ambazo hazipendelewi kutumika au kuchukuliwa, but, as they say, sometimes it is what it is. Kwahivyo, hata ukiwa wa muelekeo gani, you will be safe in our hands", alimalizia Nd. Othman.
Mwisho Nd. Othman alilielezea blog kuwa kwa Mwana-Diaspora yoyote anaetaka kujiunga na grupu hili ili apate huduma za kibenki za nyumbani, basi abonyeze link hii hapa chini.
DIASPORA BANKING NEWS:

No comments :
Post a Comment