Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, March 29, 2025

R.I.P & FAREWELL JUMA MWAPACHU

Ambassador Juma Mwapachu was simply a good man who lent his hand to the needy and his mind to the curious; he was good company, with an easy and infectious—and rather loud—laughter; he was a confident man, born of his intellect, exposure, and deeply held convictions.

He was old-school but engaged with and mastered modern times and ways with ease and comfort. He was unapologetic and non-hypocritical in the way he lived his life and expressed his opinions. He was a proud Swahili man—master of the lingo and slave of civility.

He represented the best of Tanzania and a rarity among civil servants: well-groomed, well-read, well-travelled, well-grounded, and well-spoken. He was a reluctant public intellectual. He lived a fulfilled life worthy of celebration.

He has left a mark, the most indelible one, in the hearts of the people he touched and the minds of the people he taught. Today, he took a step on the journey that we will all inevitably embark on. May his soul rest in eternal peace.

Our deepest condolences to the family!
/By an unknown author!

KUMBUKUMBU ZANGU NA JUMA MWAPACHU KUTOKA KATIKA KALAMU YAKE

Juma Mwapachu alikuwa mwanafunzi wa shule ya msingi Nansio, Ukerewe wakati Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe walipokwenda Nansio mwaka wa 1953 kumuona baba yake, Hamza Kibwana Mwapachu kuhusu uchaguzi wa TAA wa mwaka huo uliokuwa ufanyike michache michache mbele.

Abdul Sykes alikuwa anataka kauli ya mwisho kutoka kwa Mwapachu kuhusu Nyerere kuwa ndiyo Hamza hajabadili fikra yake na anamtaka Abdul ampishe Nyerere katika nafasi ya urais wa TAA?

Hamza Mwapachu alirejea katika fikra yake na akamueleza Abdul kuwa Nyerere achukue nafasi ya urais na ujao, 1954 iundwe TANU.

Juma Mwapachu kashuhudia haya kwa macho yake hakuhadithiwa.

Juma Mwapachu kasoma niliyoandika kuhusu historia ya TANU na hayo hapo chini ndiyo maneno aliyoniandikia:

''Mohamed naafiki kabisa na maelezo yako.

Ndugu Msekwa hajaandika historia ya ukweli kuhusu vuguvugu la siasa za kugombea kuelekea kuelekea uundwaji wa TANU.

Historia haifutiki wala kupinduliwa.

Hivi tatizo ni nini hasa kutoa maelezo ya ukweli?

Dr Kyaruzi alinipa nakala ya kitabu chake 'The Muhaya Doctor' baada ya kunitumia salaams kupitia kwa kaka yangu Harith Bakari kuniita niende kumuona nyumbani kwake Bukoba.

Nilikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati huo akitaka nimsaidie kuchapisha kitabu chake.

Niseme zaidi.

Muhimu ni sura moja ya kitabu hicho ikifafanua historia ya kukuzwa kwa uongozi wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mapambano yalishika moto kuanzia 1949 mjini Dar-es-Salaam.

Dr. Kyaruzi ameandika kwa makini historia hiyo.

Wewe Mohamed ni mkweli katika kunukuu historia sahihi.

Ajabu yangu Mwalimu Nyerere naye hakutaka kuandika kuhusu historia hii, kwa mfano, Nyerere baada ya harusi yake Butiama alipitia Mwanza na kuonana na rafiki yake, Hamza Mwapachu ambaye alisafiri toka Ukerewe kuonana na Kambarage kwa mara ya kwanza baada ya kurejea kutoka Scotland masomoni.

Chief Abdallah Fundikira pia alikutana na Nyerere wakati huo.

Mazungumzo yalikuwa yakimshawishi Nyerere kuongoza vita vya uhuru.

Wakati huo Edward Twinning alikuwa bado hajapiga marufuku watumishi wa serikali kujihusisha na siasa.

Lakini Twinning alitambua kwa haraka kwamba sera yake ya kuwapeleka uhamishoni mbali na Dar es Salaam wakina Hamza Mwapachu na Dr. Kyaruzi na hata Ally Sykes ilikuwa inashindwa kuzima uongozi wa siasa.

Hivi Msekwa hajui historia hii?

Na kwanini Nyerere hakutaka kuandika historia hii?

Katika mahojiano ambayo Nyerere kaweza kuongelea kuingia kwake katika siasa nasikitika kusema kwamba maelezo yake huwa mepesi au kijuujuu.

Nyerere alinipenda kama mwanawe hivyo siwezi kumlaumu.

Lakini hawa wengine kama Msekwa lazima tuwakosoe.

Wasipinde historia ya vita vya uhuru.

Nasikitika sana kwamba Hamza Mwapachu na Abdul Sykes walifariki mapema mno baada ya uhuru.

Hawa marafiki kama ndugu walikuwa hazina ya jinsi Tanganyika ilivyojiandaa na kujenga misingi ya vita vya huru.''

Mwalimu Nyerere alipata kumwambia Juma kuwa kila akimwangalia anamkumbusha baba yake Hamza Kibwana Mwapachu.
✍️...

Mohamed Said

KUTOKA MAZIKONI: CHIRAU ALI MWAKWERE, JUMA MWAPACHU NA ALLY SYKES

Ally Sykes hakupata kunieleza kama alipata kukutana na Chirau Ally Mwakwere.

Ali Mwakwere ndiyo kanifahamisha jana tukiwa Pande kumzika Juma Mwapachu.

Pande iko kilomita kiasi cha 10 kutokea Tanga mjini na ndiyo kijiji alichozaliwa Hamza Kibwana Bakari Mwapachu mwaka wa 1913.

Tuko Tanga Chumbageni nyumbani kwa kina Mwapachu msibani ni asubuhi kiasi cha saa nne visomo vimeanza.

Nimekaa na Salim Aziz tunajuana miaka mingi nilipokuwa Tanga.

Ali ananiambia Chirau Ali Mwakwere anakuja kutoka Nairobi kuhudhuria.

Salim anaendelea kunieleza kuwa yeye na Ali Mwakwere wamesoma shule moja Shimo la Tewa, Mombasa na ni mtu wake wa karibu sana.

Tukiwa pale chini akawa anawasiliana na Ali Mwakwere akamfahamisha Jumbe Menye aliyekuwa MC ajitayarishe kumpokea Muheshimiwa Chirau Ali Mwakwere muda ujao ujao.

Salim Aziz akanifahamisha usuhuba uliokuwapo baina ya Juma Mwapachu na Ali Mwakwere.

Alipomaliza mimi nikamwambia Salim Aziz kuwa mimi kisa cha Wadigo hawa wawili wasomi wa kukutana nimekipata kwa mwenyewe Juma Mwapachu.

Kisa hiki Ali Mwakwere kakieleza msibani aliposimama kutoa rambirambi na In Shaa Allah nitaweka video yake hapa mumsikie mwenyewe.

Mimi ninachotaka kukisema hapa ni kuwa Juma Mwapachu aliniambia kuwa Chirau Ali Mwakwere alishangaa na pia kushtuka kumkuta Mdigo mwezake Balozi Ufaransa.

Katika mazungumzo sasa ndiyo Juma Mwapachu akamweleza Mwakwere historia ya baba yake Hamza Kibwana Mwapachu kuwa alisoma Makerere.

Juma Mwapachu akamweleza Ali Mwakwere historia nzima ya baba yake na harakati zake katika kupigania uhuru wa Tanganyika na mchango wa baba yake kumpa Julius Nyerere uongozi wa Tanganyika.

Ali Mwakwere akamuahidi Juma kuwa yeye anakwenda kwao Kwale ambako ni mbunge na ataitisha kikao maalum kikiwa Hamza Kibwana Bakari Mwapachu apewe mtaa Kwale kama Mdigo wa kwanza kusoma Makerere.

Hili lilifanyika.
Kwale kuna Mtaa wa Hamza Mwapachu.

Tuko Pande.

Salim Aziz ananiambia, "Mohamed Ali Mwakwere kaniuliza kama umekuja mazikoni, nikamwambia mbona tulikuwa na wewe pale tumekaa pamoja?"

Kiasi cha watu wawili wakaniambia kuwa Ali Mwakwere ananitafuta.

Hapa tuko nje ya msikiti wa Pande tushasalia jeneza tunaelekea makaburini.

Hivi ndivyo nilivyokutana na Chirau Ali Mwakwere.

Mimi nikamfahamisha kuwa tulikaa jirani ndani Masjid Riadha, Lamu Maulidini mwaka wa 2009.

Ali Chirau akanifahamisha kuwa amesoma kitabu cha Abdul Sykes na chanzo chake ni Ally Sykes.

Ali Chirau anasema alikuwa Muthaiga Country Club akamuona mzee mmoja kakaa kwenye meza na mkewe.

(Hapa napenda kutahadharisha kuwa kumuona Mwafrika Muthaiga si kitu cha kawaida kwani hiyo ni "Exclusive Club" ya mamilionea).

Ali Mwakwere akanyanyuka alipokaa akaenda kumsalimia yule mzee.

Yule mzee akajitambulisha kuwa jina lake ni Ally Sykes.

Ali Chirau anasema Ally Sykes alimletea kitabu cha Abdul Sykes na ile bahasha ameihifadhi hadi leo.

Kitabu hiki kilimuathiri sana Chirau Ali Mwakwere.

Msikilize Chirau Ali Mwakwere hapo chini:

✍️...
Mohamed Said


MOYO MWEMA WA JUMA MWAPACHU

 Tulikuwa tumeshamaliza kuzika taratibu tunarudi kwenye magari yetu tuondoke Pande turejee Tanga mjini.

 Akanijia mmoja wa vijana walionipokea Tanga nilipohamia mwaka wa 1997.

 Nitamtaja kwa jina moja tu la kificho "Mwinyi."
 Mwinyi alikuwa kati ya rafiki zangu wakubwa.

 Wakati huo alikuwa mwanafunzi wa sekondari labda kidato cha kwanza.

 Mwinyi akanisalimu na kunipa pole kisha akaniuliza kama nakumbuka "note" niliyompa ampelekee Juma Mwapachu Dar es Salaam miaka mingi mingi. 

 Mimi sikuweza.

 "Nilipomaliza kidato cha nne nilitaka niendelee kidato cha tano nikaja kwako na kukueleza kuwa nyumbani hawana uwezo wa kunisomesha kidato cha tano na cha sita.

 Basi wewe ukaniandikia "note" ukanipa ukaniambia niende Dar es Salaam nikamuone Juma Mwapachu.

 Nilikwenda nikamuona na nikamweleza shida yangu.

 Juma Mwapachu ndiye aliyenisomesha hadi nikamaliza kidato cha sita."

 Nilipigwa na butwaa. 

 Vipi na iweje mimi nimesahau jambo kubwa na hisani kama hii?

 Sote tukashukuru.
 Alhamdulilah. 

 Mwinyi alipomaliza kidato cha sita aliendelea kuendelea na masomo.

 Mwinyi aliselea Uingereza kwa yapata miaka 20.

 Kamaliza masomo na akatafuta maisha huko.

 Mwaka jana nilikuwa na utafiti wa kulitafuta kaburi la Abushiri bin Salim.

 Nikaenda Tanga.
 Mwinyi akaja hoteli niliyofikia kunisalimu.

 Ndiyo alikuwa karejea nyumbani baada ya muda mrefu kupita akiwa Uingereza lakini mimi na yeye tulikuwa hatujaonana.

 Nilipomueleza safari yangu ya Pangani yeye akasema atanipeleka na gari lake.

 Tulivutana sana katika hili kwani mimi nia yangu ilikuwa kukodi gari inipeleke yeye hakutaka kunisikia kabisa.

 Si tu alinipeleka Pangani bali aliwapigia simu wahusika Pangani kuwataarifu kuwa tunakwenda kwa shughuli maalum.

 Huko kote yeye ni maarufu kwani ni mtu wa biashara. 

 Safari yangu Pangani ilikuwa na mafanikio makubwa sana.

 Baada ya mfupi nilirejea kuelekea Tanga kwenye utafiti katika utafiti wangu.

 "Sheikh Mohamed nimetingwa na kazi lakini In Shaa Allah kesho nitakuletea gari yangu na kijana akupeleke Pangani."

 Hakika nilikuwa nimeelemewa na wema na ukarimu huu.

 "Sheikh Mohamed kuna mambo mengi naona wewe umesahau."

 Tuko ndani ya gari lake yeye anaendesha mimi niko pembeni.

 "Unajua wewe ndiye uliyenifundisha mimi computer nilikuwa nikitoka shule nakuja nyumbani kwako unanielekeza.

 Kompyuta ile ilinifia mimi mikononi mwangu."

 Mimi sikumbuki haya anayonieleza Mwinyi ila naikumbuka ile computer.

 Ilikuwa zawadi kutoka kwa rafiki yangu Dr. Harith Ghassany. 

 Alininunulia tukiwa Muscat mwaka wa 1997.
 Miaka mingi imepita.

 Kama si kule kupelekwa High School na Juma Mwapachu, Mwinyi maisha yake yasingeweza hata kufika wakati wa kuendelea kuishi na masomo.

 Juma Mwapachu alikuwa na roho ya peke yake.

 Jumbe Menye aliyekuwa MC pale msibani alisema kuwa Juma Volter Mwapachu alilea vijana wengi wadogo zake.

 Hiki ndicho kisa cha rafiki yangu Mwinyi na kaka yetu Juma Mwapachu na roho yake nzuri.

✍️....
Mohamed Said

No comments :

Post a Comment