THE NEW TANZANIA IDENTITY CARDS - 2026!
Kitambulisho kipya cha NIDA Toleo la 2026 Mambo 5 mapya muhimu:
1. Kadi moja = Vitambulisho 8
Zamani kadi ilikuwa na huduma 4 tu. Sasa ina 8. Ndani yake kumeunganishwa:
- Cheti cha kuzaliwa
- Bima ya afya
- Leseni ya udereva
- TIN namba (TRA)
- Hali ya ndoa
- Kundi la damu
- Hati ya kusafiria EAC
Maana yake hutabeba tena vitambulisho 20 mfukoni.
2. Vitambulisho vya zamani BADO VINAFANYA KAZI
Usipaniki. Kama una NIDA ya zamani, usilazimishe kubadilisha. Itaendelea kutumika. Wapya ndio watapewa hii mpya.
3. NIDA Wallet App
Wamezindua App mpya. Utakuwa na NIDA yako kwenye simu, ukiitaka kuthibitisha mtu ana-scan tu simu yako. 4. Mwisho wa kutumia Namba tu ni Februari 2027
Hili ndio muhimu sana! Mkurugenzi Kaji amesema:
> "Baada ya miezi 3 kutoka sasa, hautaweza tena kutumia namba ya NIDA pekee kupata huduma. Lazima uwe na kadi ya kimwili."
Sasa hivi kuna vitambulisho milioni 1.2 vimechapwa watu hawajavichukua. Nenda kavichukue ofisi ya Wilaya ndani ya miezi 3.
5. Kama huna NIDA, hakuna NDOA
Wamesema kuanzia sasa, kufunga ndoa lazima uwe na NIDA. Pia kila mtoto anayezaliwa sasa atapewa NIDA.
Kwa ufupi: Kama bado hujachukua kadi yako, nenda kaichukue sasa. Na kama kadi yako imefutika / imechakaa, unabadilishiwa BURE bila malipo.
No comments :
Post a Comment