dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, August 10, 2012

Hotuba ya Balozi Seif kufunga mkutano wa nane wa Baraza la wawakilishi
HOTUBA YA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR, MHE. BALOZI
 SEIF ALI IDDI KATIKA UFUNGAJI WA MKUTANO WA NANE WA BARAZA LA NANE LA WAWAKILISHI, ZANZIBAR TAREHE 10 AGOSTI, 2012


Makamu wa Rais wa Pili Balozi Seif Ali Iddi
1. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uzima, afya njema na kutujaalia amani na utulivu katika Taifa letu. Naomba pia nikushukuru wewe binafsi Mheshimiwa Spika, kwa busara zako za kuweza kuliendesha Baraza lako Tukufu kwa umakini na mafanikio makubwa. Pia nawashukuru na kuwapongeza Naibu Spika na Wenyeviti wote kwa namna wanavyokusaidia

Mheshimiwa Spika katika kuliongoza Baraza hili. Vile vile, nawashukuru Wenyeviti na Wajumbe wa Kamati mbali mbali za kudumu kwa kazi zao nzuri wanazozifanya katika kufuatilia utekelezaji wa Taasisi mbali mbali za Serikali na kufanikisha mkutano huu.

2. Mheshimiwa Spika, Mkutano huu wa Nane wa Baraza la nane umekuwa wa kihistoria katika nchi yetu kutokana na mashirikiano makubwa ya Viongozi na Wajumbe wa Baraza na Watendaji wa Taasisi za Serikali. Nawashukuru wote na naomba tuendelee na mashirikiano haya mazuri.

3. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Rais wetu mpendwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa uongozi wake wa busara, hekima na unaozingatia maslahi ya wananchi. Ni dhahiri kuwa bidii za Rais Shein zinaendelea kuzaa matunda ya maendeleo katika sekta za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

 4. Mheshimiwa Spika, vile vile niwapongeze Waheshimiwa Mawaziri kwa kuwasilisha bajeti zao vizuri na kuweza kujibu hoja mbali mbali zilizojitokeza kwa umahiri na uelewa mkubwa.

5. Mheshimiwa Spika, napenda pia niwashukuru Waheshimiwa Wawakilishi wenzangu wa Baraza lako Tukufu kwa kujadili, kudadisi na hatimae kupitisha bajeti za mapato na matumizi ya Wizara zetu. Naelewa kwamba hoja zao mbali mbali walizoziibua zilikuwa na mwelekeo mzuri na nia njema ya kuisaidia Serikali yetu ya Mapinduzi ya Zanzibar. Hii imeonesha namna ambavyo Wajumbe wako walivyofahamu mafunzo mbali mbali uliyowapa. Hata wananchi wetu ambao wametutuma kuja kuwawakilisha wanafurahishwa na jinsi Wajumbe wanavyochangia na kuibua hoja mbali mbali za msingi zenye nia ya kuiletea tija nchi yetu.

 6. Mheshimiwa Spika, nampongeza kwa dhati rafiki yangu Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani, Mheshimiwa Rashid Seif Suleiman kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano na namtakia mafanikio mema katika utekelezaji wa majukumu yake ya kumsaidia Mheshimiwa Rais katika kuiongoza sekta hii muhimu ya Miundombinu na Mawasiliano. Pia nachukua nafasi hii kumpongeza aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Mheshimiwa Hamad Masoud Hamad ambae ni Mwakilishi wa Jimbo la Ole kwa ujasiri wake aliyouonesha wa kuwajibika kisiasa kufuatia ajali ya meli ya M.V Skagit. Yeye hakuhusika moja kwa moja na ajali hiyo, lakini ameona ni vyema kuwajibika kisiasa.
........................soma zaidi

Source: Zanzinews (Mapara)

No comments :

Post a Comment