dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, August 11, 2012

MAMBO MAKUBWA YAZUKA HUKO MZALENDO.NET
BALOZI SEIF IDDI ASHAMBULIWA KWA MAKOMBORA YA NYUKILIA!
Anaandika Said Sudi kuwa:
  • CCM na CUF sasa wanalindana na kuwa Wazanzibari wamekula hasara
  • A. A. Karume alikataa serikali ya GNU katika mwaka 1963 ili kuleta Mapinduzi
Zanzibar, Tanzania.
Maneno ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akilifunga Baraza La Wawakilishi kwa ajili ya Eid kuwa Mhe Hamad Masoud hakuhusika moja kwa moja na ajali ya MV Skagit yazua mzozo katika tovuti la Wazanzibari la MZALENDO.NET . Soma zaidi hapa chini maoni ya yule Mzanzibari machachari aitwae Said Sudi kama wanavyoripoti Wagagagigikoko News Network kutoka hilo tovuti la Wazanzibari.

Said Sudi 11/08/2012 kwa 6:18 um · Ingia kujibu
Dear All,
“Pia nachukua nafasi hii kumpongeza aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Mheshimiwa Hamad Masoud Hamad ambae ni Mwakilishi wa Jimbo la Ole kwa ujasiri wake aliyouonesha wa kuwajibika kisiasa kufuatia ajali ya meli ya M.V Skagit. Yeye hakuhusika moja kwa moja na ajali hiyo, lakini ameona ni vyema kuwajibika kisiasa.” Asema Balozi Seif Iddi
Kwa maneno hayo hapo juu, Wazanzibari jamani tushakwisha!
Hii ndio hatari ya GNU. Kila mmoja anamlinda mwengine. Hakuna wakutusemea sisi wanyonge pale kosa linapotokea.
Ni juzi tu rafiki yangu mmoja hapa ukumbini eti aliandika kuwa
>Sisi tukasema hata hivyo ni kuingia tu, kwani kubadilisha ukiwa ndani 
>ni rahisi kuliko kuwa nje.
Labda hapo alikusudia kuwa: kula ukiwa ndani ni rahisi kuliko ukiwa nje. This is exactly what is taking place today! Ikiwa CCM inailinda CUF na CUF inailinda CCM, sisi wanyonge jamani atatulinda nani?????
Ni kweli kabisa kama GNU imeirejesha ZNZ nyuma miaka 100, as far as democracy is concerned in our country. You don’t need to be a political scientist from Harvard University to know that governments are the limbs of nations and strong opposition parties are the brain of those limbs. Limbs without brain ndugu zanguni are valueless or to put it mildy, they won’t work with enough proficiency!
Kutegemea kwamba labda tukiingia ndani ya cabinet ya CCM tutabadilisha mambo, “ kwani kubadilisha ukiwa ndani ni rahisi kuliko kuwa nje,” ni sawa na fisi kutegemea labda mkono wa mtu utadondoka kwavile unavyo-swing sana. Hii inaitwa wishful thinking!
Let’s not forget that, here we are dealing with hard-liners. They can only understand hard-actions!
Kama ikiwa wakubwa wa CCM na CUF wanalindana kama alivyofanya Balozi Seif Iddi hapa juu, then, GNU is a great loss to the success of democracy in Zanzibar. GNU ni sawa na kuichukua mikono yako miwili na ukaifunga kamba pamoja. The result ni mkono mmoja bila ya shaka wenye nguvu kubwa – yaani nguvu za mikono miwili. Lakini nguvu zake sio za kufanya kitu cha maana. Kufanya kitu cha maana you need 2 hands to work together.
Narejea tena kuwa: Kufanya kitu cha maana you need 2 hands to work together and not 2 hands tied together. CCM and CUF are today tied together na hii ndio maana Balozi Seif Iddi anashindwa kutamka chochote hata pakitokea kosa na ndio maana japokuwa GNU inanguvu ya mikono miwili (ya vyama viwili) lakini still inashindwa kuondosha kero za wananchi ikiwemo corruption.
Eti Mikataba ya kujenga Airport ni mirathi ya zama za kale. Utamueleza nani maneno hayo na atakusikiliza? Project moja mikataba miwili na baadae tunasema eti waziri wa CUF hana sauti. Kama huna sauti unakalia nini kwenye hio cabinet? Just to be used as a playingthing by CCM????
Kwa sisi wengine tuliopoteza jamaa zetu 2001 tukitafuta haki and corruption-free ZNZ, tunasema kuwa: “ALUTA VA CONTINUA and from now onwards we will aim our guns at both CCM and CUF targets, because both CUF & CCM have lost directions and are groping in the darkness!!!”
Najua wengine wataruka na kusema eti “tizama kazi tunayoifanya Baraza la Wawakilishi!” BLW Kaka ni kama pale Hyde Park Corner kule UK. Wanabwabwaja mchana usiku wanalala!
Tukumbuke kwamba Mapinduzi ya Visiwani hayakuletwa na LEGICO!
Waingereza walitaka A.A. Karume na wenziwe wawemo katika ile cabinet ya mwanzo ya 1963 na kama wangelikubali na huku wakawa wanarambaramba asali wanayopewa basi mpaka leo tungelikuwa kule kule!!!
Kaka zanguni, take it from me – hakuna anaeramba asali na baadae akaitema!!! 


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akieleza kwenye Baraza la Wawakilishi wakati akifunga mkutano wa nane wa Baraza hilo kuwa Mhe Hamad Masoud Hamad ambae ni Mwakilishi wa Jimbo la Ole na ambae alikuwa waziri wa Mawasiliano na Miundombinu kuwa yeye hakuhusika moja kwa moja na ajali ya MV Skagit.           

Source: Geo Kimbi /Wagagagigikoko News Network                                                                                                                                                                             

No comments :

Post a Comment