Sensa Zanzibar Yaelekea Kufanikiwa
Written by Ashakh (Kiongozi)
WEDNESDAY, 29 AUGUST 2012 1
WEDNESDAY, 29 AUGUST 2012 1
Leo inaingia siku ya nne tokea kipenge cha kuanza rasmi shughuli ya kuhesabiwa watu Tanzania – sensa. Tokea Jumapili tarehe 26 August imekuwa siku rasmi kitaifa kufanyika kwa kazi ya kuhesabiwa watu. Sensa sio inafanyika kwa Tanznaia tu bali umekuwa ni utaratibu wa nchi nyingi duniani.
Baada ya kupata nafasi ya kutembelea shehia mbalimbali na kupata kuzungumza na makarani wa sensa hiyo hapa Zanzibar, wengi waliridhika na maendeleo waliyopata tokea zowezi hili kuanza. Kwa ujumla watu wengi wamekubali kuandikisha licha ya juhudi za kutaka kususia zowezi hili.
Karani wa uandikishaji shehia ya Kikwajuni-Chini elieleza mafanikio aliyopata tokea siku ya mwanzo hadi leo hii kuwa ametembelea nyumba 62 katika shehia ya eneo la kazi yake. Ndani ya idadi ya nyumba hizo, ni nyumba mbili tu ndio zilizokataa kutoa ushirikiano. Baada ya kuwasilisha taarifa yake kwa sheha wa Shehia ya Kikwajuni Chini, nyumba moja baadae ilikubali kujiandikisha.
Taarifa zote za nyumba zilizokubali na zile zisizokubali huwa zinawasilishwa kwa Sheha wa Shehia. Pale inapohitajika busara zinatumika kwenda kuzungumza na wananchi na kuwanasihi.
Pamoja na taarifa zisizo na uhakika, hata wale walikuwa mstari wambele kupinga sensa wameweza kuhesabiwa. Hii inaonyesha kwamba sensa inaendelea kufanikiwa.
Sensa inatumika katika nchi zote dunia kutabua idadi ya wananchi wake, wanaojuwa kusoma na kuandika pamoja na kiwango cha elimu, wenye ajira na wasio na ajira, walemavu, wanawake na wanaume, na mengieo. Taarifa hizi zinakuwa ni muhimu kuisadia serikali pale inapotaka kupanga mipango yake kwa ile fani inayohusika. Mfano pale inapotaka kujuwa idadi ya wanafunzi inakuwa rahisi kupanga mahitajio yao. Tokea vitabu, walimu, na vifaa vyengine.
Chanzo: Mzalendo.net
Kwa hilo tunashukuru!
ReplyDelete