dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, August 7, 2012


SMZ KUWAOMBA RADHI MABALOZI

Written by Ghalib  //  06/08/2012 

Waziri Mohammed Aboud
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeomba radhi kufuatia baadhi ya mabalozi wa nchi za kiarabu waliopo Zanzibar kuzuiliwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Amani Abeid Karume mjini Zanzibar.
Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais Mohammed Aboud amesema serikali itawahakikishia mabolozi waliopo Zanzibar na kutoka nchi nyingine kitendo kama hicho hakitatokea tena.

Amesema wafanyakazi waliofanya vitendo hivyo watashughulikia ili kuona heshma na nidhamu inaendelea kuwepo kwa viongozi hao wa kimataifa walioletwa na nchi zao kudumisha ushirikiano
Awali mwakilishi wa jimbo la Kwamtipura Hamza Hassan Juma alitishia kuzuwia kifungu cha fedha cha wizara ya miundo mbinu na mawasiliano wakati wakupitisha bajeti ya wizara hiyo akitaka serikali kutoa kauli juu ya kitendo cha kufungiwa geti maafisa hao wa kibalozi katika uwanja wa ndege wa Zanzibar.

Hata hivyo Juma ameitaka serikali kuheshimu sheria katika uteuzi wa viongozi wa mamlaka za taasisi za serikali badala ya kutumia utashi binafsi.

Source: Mzalendo.net

No comments :

Post a Comment