Utaratibu mpya wa Sumatra wasotesha abiria bandarini
15th August 2012
Kwa mujibu wa utaratibu, abiria haruhusiwi kukata tiketi ya kusafiri kwenda visiwani humo iwapo hatakuwa na kitambulisho, kikiwamo cha uraia.
Vitambulisho vingine ambavyo abiria anatakiwa kuwa na kimojawapo, ni pamoja na cha makazi, kupiga kura, kazi, leseni ya dereva, utambulisho kutoka serikalini au pasi ya kusafiria.
Baadhi ya abiria waliokwama kusafiri, walisema wamechelewa kupata taarifa hizo kwa kuwa hawaujasikia utaratibu huo katika chombo chochote cha habari.
Utaratibu huo ambao maelezo yake yamebandikwa kwenye kuta za ofisi za kukatia tiketi katika bandari za meli zinazokwenda visiwani humo, umeelezwa kuwa ulianza kutumika rasmi Agosti 13, mwaka huu.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment