dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, August 8, 2012

Wizara kukatwa bajeti kuchangia 
ununuzi meli mpya

Na Mwantanga Ame
MAFUNGU yaliyofutwa katika bajeti ya Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kutoka Idara ya Ushirikiano wa kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi nchi za nje, yatatumika kwenye ununuzi wa meli.

Serikali imechukua hatua hiyo baada ya hapo awali kulazimishwa kuondolewa kwa mafungu hayo baada ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoridhika na matumizi yake jambo lililomfamya waziri wa wizara hiyo Mwinyihaji Makame kukubali kuondolewa matumizi yake.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf Mzee, aliahidi kuona mafungu hayo yanatumika kwa shughuli za serikali ndani ya bajeti yake mpya.

Waziri Omar, wakati akiwasilisha bajeti kwa mwaka wa fedha 2012/2012, katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea Mjini Zanzibar, alisema mafungu hayo yenye thamani ya shilingi milioni 40 yatahamishiwa katika ununuzi wa meli mpya ya serikali.

Alisema wizara hiyo ili kuweza kutekeleza amri ya Rais kuweza kununua meli hiyo, inakusudia kuchukua mkopo kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar na kuongeza kiwango cha mkopo wa ndani kutoka PBZ na ZSSF.

Pia Waziri huyo alisema utekelezaji huo utaweza kufanya marekebisho ya Bajeti kwa kubana matumizi ya kawaida kwa baadhi ya vifungu kwa wizara zote ili kuongezea kufikia kiwango kitakachohitajika baada ya kufahamika gharama halisi.

Akizungumzia mapato, alisema serikali imefanikiwa kuongeza mapato na kuidhinisha miradi ya maendeleo 24 yenye thamani ya dola za kimarekani 139.38.

Waziri huyo alisema maeneo mbali mbali ya ukusanyaji wa mapoto ya serikali yanaridhisha baada ya kuonesha ufanisi huku uwekezaji ukiongezeka pamoja na kwenda sambamba na uimarishaji wa huduma za fedha katika mabenki.

Waziri huyo alifahamisha katika mwaka wa fedha uliopita, Bodi Mapato Zanzibar (ZRB), imeweza kufikia shilingi 120,500 milioni ikiwa ni sawa na asilimia 100.6 ya makadirio ya mwaka.

Kutokana na hilo waziri huyo alisema kwa mwaka ujao wa 2012/2013 itakusanya jumla ya shilingi 162,000.0 milioni, ikiwa ni ongezeko la asilimia 35 ikilinganishwa na makusanyo halisi ya mwaka 2011/2012.

Upande wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), alisema mpaka kufikia Juni 30, TRA ilikusanya jumla ya shilingi 91,170.0 milioni sawa na asilimia 91 ya lengo ambapo kiwango hicho kinaashiria ukuaji wa mapato wa asilimia 20 ikilinganishwa na mapato halisi ya shilingi 76,360.0 milioni yaliyokusanywa mwaka 2010/11.

Akizungumzia juu ya Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ), alisema mwaka 2011/12 imeweza kupokea amana za wateja zenye kima cha shilingi 59,950.0 milioni ikiwa ni asilimia 92 ya lengo lililowekwa la shilingi 65,430.0 milioni, na kutoa mkopo wa shilingi 66,300.0 milioni sawa na asilimia 178 ya lengo lililowekwa la 37,060.0 milioni kwa mwaka.

Waziri Omar alisema hali hiyo imeweza kuongeza rasilimali ya benki za shilingi 76,450.0 milioni ikilinganishwa na lengo la shilingi 100,000.0 milioni na kupata mapato ya shilingi 18,660.0 milioni yanayotokanayo na huduma mbali mbali za kibenki ambayo ni sawa na asilimia 113.3 ikilinganishwa na makadirio ya shilingi 16,480.0 milioni.

Akizungumzia mfuko wa Hifadhi ya Jamiii Zanzibar (ZSSF), alisema unaendelea kuongeza wanachama wa mfuko huo ambapo hadi sasa wamo katika hatua ya kupata mshauri elekezi kwa ajili ya kuufanyia mageuzi Mfuko ambapo kampuni ya Muhanna & Co. Actuaries & Consultant imeteuliwa kuifanya kazi hiyo.

Alisema pia mfuko huo hivi sasa unajipanga kutekeleza matayarisho ya ujenzi wa kiwanja cha kufurahishia watoto Kariakoo na ujenzi wa nyumba za bei nafuu.

Waziri huyo ameliomba Baraza hilo kwa mwaka wa fedha wa 2012/13 kumuidhinishia ukusanyaji wa mapato ya shilingi 343.45 bilioni na matumizi ya jumla ya shilingi 130.760 bilioni.

Alisema kati ya fedha hizo ikiwa ni shilingi 39.584 bilioni ni kwa kazi za kawaida na shilingi 38.352 bilioni kwa ajili ya kazi za maendeleo kwa Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, na shilingi 52.824 bilioni kwa matumizi ya Mfuko Mkuu wa serikali.

Imewekwa na MAPARA /ZANZINEWS

No comments :

Post a Comment