Marehemu Daud Mwangosi
3rd August, 2012.
Walioshuhudia kifo cha Daudi Mwangosi waelezea walichokiona;
Kauli ya Chagonja; LHRC/Dkt. Kijo-Bisimba wasema "Tumechoka kutoa matamko, Sasa tutaishitaki nchi Kimataifa"
Baada ya vifo kadhaa kutokea Tanzania na wananchi pamoja, asasi na wanaharakati kutoa matamko mbalimbali yakielekezwa kwa Serikali na vyombo vyake, lakini hatua zinazochukuliwa ikiwa ni pamoja na uundwaji wa tume za kufanya uchunguzi ambazo hutoa ripoti ama zisizoridhisha wananchi au zisizokidhi haja pasina tashwishi, shirika la Haki za Binadamu limekaa na kukusudia kuachana na utoaji matamko na badala yake kuchukua hatua ya ya kuishitaki Serikali katika vyombo vya Kimataifa.
Kufuatia kifo cha mwandishi wa habari na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Iringa (IPC), marehemu Daudi Mwangosi chama hicho mkoa kikieleza kushauriana na jukwaa la wahariri nchini kimetangaza kususia kazi za Jeshi la Polisi mkoani humo hadi watakapokuwa wametoa taarifa za kweli dhidi ya wahusika na kuacha propaganda juu ya tukio hilo.
Kifo cha Daudi Mwangosi - Dina Chahali, Chief News Editor, Channel TEN
Source: Wavuti
No comments :
Post a Comment