Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, September 22, 2012

MSAADA KUTOKA WANA-DIASPORA WA CANADA (ZACADIA)

Zanzibar-Canadian Diaspora Association


DATE: SEPTEMBER 21, 2012.

Kuh: MTOTO NAIRAT NA DADA YAKE

Wazanzibari wanaoishi Canada ambao wanajumuika pamoja chini ya Jumuia yao ijulikanayo kama ZACADIA (Zanzibar-Canadian Diaspora Association) wameshitushwa na kusikitishwa na hali ya kiafya ya mtoto Nairat na dada yake pamoja na familia yao nzima kwa ujumla - kama walivyosoma huko nyuma kwenye ukumbi huu <http://www.zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2012/08/please-help-this-kid-mtoto-nairat-seven.html>.

Kutokana na hali hio mbaya ya kiafya ya watoto hao, ZACADIA katika kusaidia matibabu ya Nairat na dada yake inatoa mchango wake wa TShs 750,014.04

Pesa hizo zimepelekwa Zanzibar tarehe 21 September, 2012 kutoka Canada kwa njia ya MONEYGRAM, kupitia  kwa Bi Salma Said ambae ni mdhamini wa hawa watoto kwa hivi sasa.
Kwa niaba ya Wana-Zacadia wote waishio Canada tunamtakia mtoto Nairat pamoja na dada yake shifaa ya haraka na kwa wakati huo huo tunaitakia Zanzibar kila mafanikio katika wakati huu mgumu wa kiuchumi kwa Ulimwengu mzima.

Kila la kheri.

Hassan Othman
Katibu / ZACADIA (Toronto, Canada).


No comments :

Post a Comment