Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, September 4, 2012

Taarifa Kwa Umma - Jeshi La Polisi Lakanusha Watoto Kuhudhuria Shule Wakiwa Gerezani Kwimba



JESHI LA MAGEREZA LAKANUSHA HABARI YA WATOTO KUHUDHURIA SHULE WAKIWA GEREZANI KWIMBA.

Na: Veronica Kazimoto – MAELEZO
Dar es Salaam
4/09/2012.
Jeshi la Magereza nchini limekanusha habari kuwa kuna watoto katika Gereza la Wilaya ya Kwimba wanaoenda shule na kurudi gerezani kuungana na familia yao.

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamishna Jenerali wa jeshi la Magereza nchini Fideli Mboya, kufuatia habari 


iliyotolewa na Gazeti moja la kila siku hapa nchini, kuwa kuna watoto Gereza la Kwimba ambao wanahudhuria masomo huku wao na wazazi wao wakiwa gerezani.
“Yote yaliyoelezwa kwenye habari hiyo yana ukweli isipokuwa suala la watoto kuhudhuria masomo wakati wakiwa gerezani,ukweli ni kwamba hakuna watoto wanaotoka gerezani hapo kwenda shule na kurudi gerezani”, imeeleza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ya jeshi la Magereza nchini imeeleza kuwa, kuna familia ya watu watano baba, mama na watoto watatu wenye umri wa miaka 20, 19 na 1 ambao wote ni washtakiwa wa kesi ya mauaji isipokuwa huyo wa umri wa mwaka mmoja.
Katika taarifa yake kaimu Kamishna Mboya ameeleza kuwawatuhumiwa wote wapo gerezani wakisubiri upepelezi wa kesi yao ya mauaji inayowakabili ukamilike na hakuna kati yao anayetoka nje ya gereza na kurudi kama mtu huru.
Jeshi la Magereza nchini limelazimika kutoa ufafanuzi wa taarifa hii kufutia mbunge wa viti maalum mkoa wa Mwanza Leticia Nyerere kufanya ziara katika gereza la wilaya ya Kwimba na taarifa za ziara hiyo kuchapishwa katika gazeti moja la kila siku hapa nchini.


WAGAGAGIGIKOKO NEWS NETWORK (WANENE)
WAMEZIBLOCK HIZI HABARI ZISITOKE KUTOKANA NA UNYAMA WALIOUFANYA POLISI WA TANZANIA KWA NDUGU YETU DAUDI MWANGOSI.
TUTAENDELEA KUTOTOWA HABARI ZOZOTE ZINAZO HUSU VYOMBO VYA USALAMA NCHINI MPAKA WIKI YA MAOMBOLEZI IISHE!!
BADO TUNAENDELEEA KUWALAANI POLISI WA TANZANIA KWA UNYAMA WALIOUTENDA KWA MTANAZNIA MWENZETU!
SAMAHANI KWA WAPENDA AMANI WOTE WA NCHI HII.
MOLA AMLAZE MAREHEMU PEMA PEPONI. AMEN!


No comments :

Post a Comment