Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, September 28, 2012

UAMSHO NA SIASA ZANZIBAR!!!

UAMSHO YABAINISHA SABABU ZA MASHEHE KUSHIRIKI KUDAI UHURU WA ZANZIBAR

Written by   //  28/09/2012  
waislamu na waznzibar kote nchini wametakiwa kufuata mfumo aliouweka Allah kwa waja wake kwa lengo la kupata mafanikio mema hapa duniani na kujiepusha na adhabu huko akhera
wito huo umetolewa leo na shekh Khalfan  Nassor katika mhadhara uliofanyika katika viwanja vya masjid salami magogon wilaya ya maghrib unguja. Aidha amewasihi viongozi walioko madarakan kutumia madaraka yao kwa uadilifu na kulinda haki za wale wanaowaongoza na kusisitiza kuwa mashehe hawana nia ya kuwaondosha madarakani katika nyadhifa zao bali  ni jukumu lao kufikisha ujumbe wa allah kwa waumin wote wakiwemo na viongozi. 

kwa upande wake amir wa jumuiya na taasisi za kiislamu hapa nchini shekh Mselem bin Ally amesema suala la kudai hadhi na maslahi ya zanzibar kuwa huru sio jambo rahis na kuwa linahitaji ustahmilivu mkubwa, hata hivyo amewataka vijana kuwa makini juu ya kile alichokiiita kuwepo kwa njama za kuvuruga harakati zao za kudai uhuru wa zanzibar zinazofanywa na wasioitakia mema zanzibar. 
Akibaanisha sababu ya mashehe kushiriki katika kudai uhuru wa zanzibar ni kuwasaidia viongozi wenye uchungu na nchi yao kwani wanaonekana kukosa nguvu na ushirikiano kutoka kwa baadhi ya viongozi katika serikali ya umoja wa kitaifa zanzibar, hivyo amesema hata zile sababu za kuanza kwa upinzani wa vyama zanzibar kulikua ni ile ile kuitakia mema nchi, kutokana na kushindikana kwa wanasiasa wakuitetea zanzibar ndio maana wananchi wenyewe wameamua kufanya jitihada na juhudi za kuikomboa nchi yao.

Chanzo: Mzalendo.net

No comments :

Post a Comment