ZITTO AROPOKWA TENA!!!
Hii hapa chini ni barua iliyotoka kwenye ukumbi mmoja unaoitwa WANABIDII, kuhusu hii mada ambayo ilianzishwa na ZANZIBAR NI KWETU. Katika majadiliano yanayoendelea huko kwenye huu ukumbi, kuna kaka mmoja anaeitwa Bart Mkinga alitoa msg yake ya hapa chini hapo tarehe 29 September, 2012.
Kwa kweli tumefurahishwa na maelezo yake ya kijitu kizima na ukweli alioutoa. Kabla ya kuitoa hii barua yake hapa kwenye blog letu ilibidi tumuulize kwanza kama angependelea tufanye hivyo. Hii ndio kawaida, lakini wakati mwengine mambo yanavyonoga vizuri inabidi kawaida uiachie pembeni.
Kwahivyo, Kaka Bart tunakuomba radhi na kwa mara hii utustahamilie na utusamehe. Tunakuahidi kuwa haitotokea tena, unless labda ulete ukweli mwengine kama huu wa kutufungua macho yetu zaidi!
Tumeitoa hii barua ya Kaka Bart hapa chini kwasababu wengine hawajui kuwa urais wa nchi sio cheo, bali ni kazi ngumu sana na kwa dunia ya leo mtu kuikimbilia kazi ngumu inabidi tumtizame kwa macho yetu yote mawili!
Hakuna ambae hajasikia uvumi kwamba Mzee Makamba anamfanyia kampeni za chini chini January ya kuwa Rais - hatujui katika mwaka gani, lakini ona January alivyojibu wakati alipoulizwa juu ya nia hio!
Zitto inaonesha hana watu wa karibu wakumu-advise juu ya nini aseme na nini asiseme na hii haitomfikisha mbali. Na hata kama akiwa nao watu wakumu-advise, hatudhanii kama atawasikiliza. Mwenzetu ni mjuwaji kidogo na hapendi kuenda sambamba na wenzake. Hii nayo pia sio sifa ya kujivunia!
You might have all the ammunition at your disposal, but if you don't know how to shoot, then, you are .................(malizia mwenyewe!)
Hakuna ambae hajasikia uvumi kwamba Mzee Makamba anamfanyia kampeni za chini chini January ya kuwa Rais - hatujui katika mwaka gani, lakini ona January alivyojibu wakati alipoulizwa juu ya nia hio!
Zitto inaonesha hana watu wa karibu wakumu-advise juu ya nini aseme na nini asiseme na hii haitomfikisha mbali. Na hata kama akiwa nao watu wakumu-advise, hatudhanii kama atawasikiliza. Mwenzetu ni mjuwaji kidogo na hapendi kuenda sambamba na wenzake. Hii nayo pia sio sifa ya kujivunia!
You might have all the ammunition at your disposal, but if you don't know how to shoot, then, you are .................(malizia mwenyewe!)
By 2012/9/29 Bart Mkinga
Kuna haki na uhuru wa kufanya jambo, halafu kuna busara ya kufanya jambo. Nina uhakika kabisa kuwa Zitto ametumia haki na uhuru wake wa kikatiba (katiba ya Jamhuri ya Tanzania na katiba ya chama) lakini nahisi hakutumia busara.
Bado nashikilia kauli ya Mwalimu, mtu anayeutaka sana Urais -------------, ni wa kumwogopa kama ukoma. Nafurahia sana utaratibu wa FRELIMO wa vikao vya chama kumpendekeza mtu wanayedhani anafaa kuwa mgombea wa kiti cha Urais badla ya mtu kujipendekeza mwenyewe. Ni kwa kupitia utaratibu huu, haishangazi kuona Joachim Chisana alitangazwa kuwa Rais bora mstaafu.
Pamoja na CHADEMA kuungwa mkono na Watanzania walio wengi lakini ni ukweli pia kuwa bado ni kichanga. Na sidhani kama kina uwezo mkubwa wa kuhimili migawanyiko ya makundi ambayo yanaweza kuundwa na viongozi wake wakuu (Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, n.k.) kwa nia ya kuutaka Urais. Lililo muhimu kwa sasa ni kwa viongozi wa juu wa CHADEMA kushikamana ili watakapomtoa mgombea kupitia CHADEMA awe ni mwakilishi halisi wa CHADEMA, na siyo mwakilishi wa kundi ndani ya CHADEMA.
CCM, pamoja na ukongwe wake, makundi ya Urais yamekidhoofisha kwa kiasi kikubwa. Kigwangala na wengineo wa CCM watafurahia sana wakiona kuna makundi yanajengeka ndani ya CHADEMA.Ni lini Kigwangala alisifia jambo jema ndani ya CHADEMA? Kwa nini leo watu wa kwanza kuisifia kauli ya Zitto wawe ni CCM?
CHADEMA kikitaka kupata mafanikio katika uchaguzi Mkuu, kwa sasa viongozi wake wajishughulishe zaidi kujenga chama, kutoa elimu kwa wapiga kura, na kujenga mfumo imara na wa kidemokrasia ndani ya chama. Kiongozi yeyote ambaye atajishughulisha zaidi kujenga makundi ya Urais badala ya jukumu la msingi, ni adui wa maendeleo ya harakati za kuleta mabadiliko. CHADEMA ikifanya kosa la kuwaacha viongozi wake kuufikiria Urais zaidi kuleta harakati za utoaji Elimu kwa wapiga kura, hata wakipata dola, hawatakuwa tofauti na CCM, watalazimika kuyahudumia makundi badala ya Watanzania, na kwetu sisi kilicho muhimu siyo Zitto, Dr. Slaa, Mh. Mbowe, n.k. kuwaona mmojawapo akiwa Rais, bali ni kujiuliza kuwa huyo atakayekuja kuwa Rais ataleta kitu gani kipya kiutawala, kimfumo, kisera, kiutendaji na katika usimamizi wa majukumu ya serikali. Na kama tunataka hilo, ni lazima tofauti yake ianze kuonekana kuanzia kwenye mfumo wa upatikanaji wa wagombea wenyewe. Taratibu wanazozishabikia akina Kigwangala ndiyo zilizotuzalishia viongozi wa namna ya sasa, viongozi ambao wameshindwa kutoa matumaini kwa watanzania, na kubakia kuwa watumwa wa makundi yaliyowapeleka kwenye utawala.
Sina tatizo na Zitto kuwa mgombea wa CHADEMA au mwananchi yeyote lakini siungi mkono nguvu kubwa anayotumia kuwaaminisha watu kuwa yeye ndiye pekee mwenye uwezo huo. Tamaa yake kubwa inanipa mashaka makubwa. Je, tamaa hiyo yote dhamira yake ni kuwatumikia Watanzania au ni nia ya kufikia tamaa yake ya kimaisha. Angalizo ni kuwa watu wanaoyapenda sana madaraka, hawajawahi kuwa viongozi bora, na kuna wakati walipoyapata waligeuka kuwa madikteta, kiasi cha kukataa kuondoka madarakani baada ya muda wao kwisha.
Naikumbuka hotuba ya Hayati Mwalimu Nyerere pale UDSM kwenye kongamano la "Hatma ya Uongozi wa Afrika', akimjibu aliyemwuliza, 'ni nini sifa za kiongozi mzuri', mwalimu alimjibu akinukuu maneno ya Mwanafasafa mmoja, 'kiongozi mzuri ni mwanafalsafa lakini tatizo la wanafalsafa ni kuwa hawapendi kuwa viongozi mpaka walazimishwe, matokeo yake ni kuwa wengi wa wanaoutaka uongozi huwa ni wale wasiofaa'. Kwetu Watanzania, baada ya kupitia kwenye uongozi wa kila aina ambao umeshindwa kuleta tija, inabidi tujiulize, 'Je, ni nani miongoni mwetu afaaye kuwa kiongozi, hata kama hataki kuwa kiongozi, tumwombe/tumlazimishe awe kiongozi wetu', maana wengi wa hawa wautakao uongozi wanautaka kwaajili ya utukufu wao. Na tumewaona wengine wakitamka wazi kuwa Urais ni wa kwao na familia zao, na katika hilo hawana ubia na mtu mwingine, maana yake ni kuwa hawana ubia na Watanzania, wakati ukweli ni kuwa uongozi unastahili kuwa wa Umma, siyo wa mtu au kikundi cha watu, wabia wakuu wa uongozi wowote ulio makini lazima wawe wale unaowaongoza.
Bart
No comments :
Post a Comment