HARAKATI YA UAMSHO YASEMA INASHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI KUMTAFUTA AMIRI FARIDI
Wana-Uamsho
Written by Harith // 17/10/2012
HALI YA TAHARUKI IMETANDA KATIKA MAENEO YA MKOA WA MJINI MAGHARIBI BAADA YAKUENEA KWA TAARIFA ZAKUKAMATWA NA KUTEKWA NYARA NA WATU WASIOJUILIKANA MSEMAJI WA JUMUIYA NA TAASISI ZAKIISLAM ZANZIBAR AMIRI FARID HADI AHMED.
WAFANYABIASHARA WA MAENEO YA DARAJANI MJINI ZANZIBAR WAMEKUFUNGA MADUKA YAO WAKIHOFIA VITENDO VYA VURUGU VILIVYOANZA KUTOKEA KUFUATIA KUKAMATWA KWA KIONGOZI HUYO.
BARABARAZA ZOTE ZA MAENEO YA MJINI ZIMEWEKWA MAWE NA KUCHOMWA MIPIRA YA GARI ILITOA MOSHI MWEUSI ULIOENEA KATIKA MAENEO MBALI MBALI YA MJINI NA HADI KUFIKIA AMANI KATIKA MAKUTANO YA BARABARA INAYOTOKEA UWANJA WA NGEGE KUELEKEA MTONI NA MWERA.
VIJANA WA MAKUNDI MAOVU YA UBAYA UBAYA NA MBWA MWITU WAKIWA NA MAPANGA WALIFANIKIWA KUJIINGIZA KATIKA KUNDI LA WAFUASI WA UAMSHO WALIKUWA WAKIDAI KUACHIWA KWA SHEIKH FARIDI WAMEVUNJA BAA KADHAA ZA MAENEO YA MJINI NA WILAYA YA MAGHARIBI.
VIJANA HAO WALIOJINASIBISHA NA UAMSHO WALIKUWA WAKINYWA POMBE NJIANI BAADA YAKUKIMBIA NA KRETI ZA BIA NA BAADAE KUZIVUNJA KATIKA MAENEO YA BARABARA ZA DARAJANI NA MJI MKONGWE WA ZANZIBAR.
POLISI WAKUTULIZA GHASIA WALIFANIKIWA KUTULIZA VURUGU HIZO MAJIRA YA JIONI BAADA YAKURUSHA GESI YA KUTOA MACHOZI NA KUWATAWANYA WAFUASI WA HARAKATI YA UAMSHO WALIOKUWA WAKIDAI KUACHIWA KWA KIONGOZI WAO.
AKIZUNGUMZA NA RADIO NOOR FM AMIRI MKUU WA JUMUIYA NA TAASISI ZAKIISLAM ZANZIBAR SAMAHATU SHEIKH MSELLEM BIN ALI AMETHIBITISHA KUTEKWANYARA KWA KIONGOZI HUYO NA KUONGEZA KUWA WANASHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI ZANZIBAR KUMTAFUTA.
AIDHA SHEIKH MSELLEM AMETOA MUDA WA SAA 24 KUACHIWA KWA KIONGOZI HUYO ALIYEKAMATWA NA WATU WASIOJUILIKANA KABLA YA HARAKATI YAKE HAIJACHUKUWA CHUKUWA HATUA ZINAZOFAA.
WAKATI HUO HUO NAKO MJINI DAR-ES-SALAAM KUMERIPOTIWA KUTOKEA MAANDAMANO NA VURUGU KADHAA ZA WAISLAM BAADA YA JESHI LA POLISI KUMKAMATA AMIRI WAKUTETEA HAKI ZA WAISLAM TANZANIA SHEIKH PONDA ISSA PONDA.
Chanzo: Mzalendo
No comments :
Post a Comment