Hakuna mjadala kuhusu Visiwa vya Zanzibar Muhimu ni kutafuta uhuru wa kisiasa kwanza
Na, Khaleed Gwiji Zanzibar
Ni ukweli usiopingika kuwa visiwa vya Unguja na Pemba ambavyo
kwa muda wote wa historia vimekuwa PACHA wasiotengana -
na ambavyo watu wake wanachangia historia moja na
khatima moja kama Wazanzibari - vina rasilimali nyingi za
kiuchumi za ardhini na baharini ambazo zinaweza
kutumiwa kwa maendeleo endelevu ya taifa letu kimsingi
kielimu na kiuchumi. Hakuna mjadala kuhusu Visiwa vya
Zanzibar kuwa na hali nzuri kiuchumi. Muhimu ni
kutafuta uhuru wa kisiasa kwanza.
Chini ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar yenye mamlaka kamili
kitaifa na kimataifa - Zanzibar tutaitangaza kuwa ni
BANDARI HURU na kuifanya iwe ni kituo cha kikanda
na cha kimataifa cha kibiashara na kituo cha teknologia
na mawasiliano na kiuchumi ambao utatumia Dola ya
Kimarekani ambayo tayari ni sarafu ya pili katika
mabadilishano ya kifedha Zanzibar hata katika matumizi
ya kawaida.
Maurituis ambayo ni sawa na Zanzibar KIENEO - sasa
inachukuliwa kama mfano mzuri wa Afrika katika
maendeleo ya kielimu, kiuchumi na kijamiii.
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar - KWANZA !
Chanzo: Swahilivilla
No comments :
Post a Comment