Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, November 24, 2024

MJI MKONGWE - KWA HILI LIFIKIRIENI TENA!


Dear Ndugu Mkurugenzi,
Sote tunaziona juhudi na jitihada zako za kuufufuwa Mji wetu Mkongwe.
Sote tunafurahi sana kwani safari yako imefika mbali.
Kazi zako nzuri zinaonekana na kila Mzanzibari.
Mji wetu Mkongwe leo unang'ara na kwa hili tunakuvulia kofia na tunakupa HONGERA!

Kuupaka Mji Mkongwe wote rangi ni jambo zuri sana na kila Mzanzibari anafurahia jambo hili, kwani Mji Mkongwe ni taa ya Zanzibar yetu. Lakini, kwa upande wapili wengine tunaona kutoa service hii bure kwa majumba yote ni sawa na kupoteza the meagre resources available at your end. Hii ni kwasababu kuna wamiliki wengine wa majumba haya wenyewe wangeweza kuyatia rangi majumba yao hata kila baada ya miezi sita kama Mamlaka yako ingetoa Muongozo huo, kwani majumba haya yanakodishwa kwa kodi ambazo hazisemeki kwa ukubwa na kuyapaka bure rangi ni kupoteza resources - kwasababu wamiliki wanao uwezo huo!

Mkurugenzi, bora hizi gharama wanazozitoa Infinity na nyinyi wenyewe zingelitumika kwa mambo mengine kadhaa ambayo hayapo kwenye Mji Mkongwe, kuliko kuzipoteza kwa kutoa service ya bure kwa wenye uwezo na wasiostahiki.

Mamlaka inaweza kuweka by-law ya kuwa kila jumba la Mji Mkongwe kila baada ya miaka 2-3 litiwe rangi na wasiotia rangi wapelekwe mahakamani na wapigwe fine na Mamlaka iitumie hii fine kulitia jumba rangi.


ABOVE: ZANZIBAR's OLD TOWN (MJI MKONGWE)

Hatutaki Mamlaka itufahamu wana-blog la ZNK vibaya. Hatupingi kutiwa rangi majumba ya Mji Mkongwe. Pia, hatupingi kusaidiwa wasiojiweza. Tunachopinga ni kuwapa service ya bure wengi ambao hawastahiki na kama hio rangi ndio imepatikana kwa msaada kutoka Infinity basi Mamlaka tarehe 2 December itoe tamko rasmi kuwa ita-evaluate majengo yote ya Mji Mkongwe na yatakayoonekana kuwa ni machafu basi Mamlaka itayatia rangi na wamiliki watapelekewa bill, Full stop!

Zipo njia nyingi za kupata fedha za maendeleo au kama alivyoandika mhenga mmoja kuwa...."Much can be done with limited resources but with unlimited imaginations"!


2 comments :

  1. Duh! ZNK mmefikiria mbali. Ni kweli kuyatia rangi majumba yote ya Mji Mkongwe ni ubadhirifu hata kama hio rangi ni ya bure. Baadahi ya nyumba za Mji Mkongwe zinakodishwa zaidi ya Dollar za Mmarekani 6,000 kwa mwezi. Kuzitia rangi nyumba hizi sio haki. Mnamengi Mji Mkongwe yakufanya. Yauzeni hayo ma-container ya rangi mliopewa bure ili mpate pesa ya mambo mengine muhimu. Kupanga ni kuchaguwa. Chaguweni ya maana zaidi!

    ReplyDelete
  2. Rais kaweka wazi tarehe 2 Dec kuwa zitakarabatiwa nyumba za wale watu ambao hawaba uwezo na sio vile alivyosema Mkurugenzi kuwa ni nyumba zote. ZNK you had every right to get concerned. Mkurugenzi alikuwa hakuweka wazi lakini Rais Mwinyi kaweka wazi na sote tumefahamu sasa.

    ReplyDelete