KUJIUZULU KWA MHESHIMIWA JUSSA SI MGOGORO WALA KUYUMBA KWA CUF
Written by Ahmed Omar Khamis // 05/10/2012 //
Kujiuzulu ni jambo la kawaida lakini tu katika taasisi iliyopevuka kidemokrasia na kiuwajibikaji. Hii ndio maana si jambo la kawaida katika vyama vyote vya siasa hapa nchini ukiwachia CUF. Mheshimiwa Jussa amejitathmini na kujiona kuwa chama kimemkabidhi majukumu mawili makubwa, Mtendaji Mkuu wa chama kwa upande wa Zanzibar na Mpambanaji katika baraza la wawakilishi. Majukumu haya mawili na ukubwa wake kwake ni sawa na aliyepanda farasi wawili, atachanika msamba au farasi mmoja atashindwa kumdhibiti na bila shaka atakimbia.
Ili kukinusuru chama na kuzorota kiutendaji katika nafasi muhimu na kubwa kiutendaji kwa Zanzibar ya Naibu katibu Mkuu, Mhe Jussa ameonelea ni vyema akamwachia mwenzake nafasi hiyo ili yeye apate muda wa kutosha kukiwakilisha chama katika Baraza la wawakilishi akiwa GREAT CHAMPION katika kuibana serikali na kuyawakilisha matashi ya wazanzibari vile ambavyo wanatarajia. Yaani kuidai na kuileta Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Kujiuzulu kwa Mhe Jussa ni kuona na sio kuyumba.
Chanzo: Mzalendo
No comments :
Post a Comment