- Ponda alikamatwa mida ya saa 5 usiku muda ambao unahisiwa kuwa sawa na ambao mwenzake Sheikh Farid wa Uamsho (Zanzibar) anadaiwa kupotea; unaweza kufuatilia - Sheikh Farid wa Uamsho 'atekwa nyara' visiwani Zanzibar
- Wafuasi wa Ponda wameanza purukushani, unaweza kusoma - Hali tete Central Police Dar; wafuasi wa Sheikh Ponda waanzisha purukushani!

KAULI YA KAMANDA KOVA:

Quote By Uswe View Post
Kamanda Kova akiongelea sakata la kukamatwa kwa bwana Ponda na maandano ya waislamu waliokuwa wanajaribu kushinikiza bwana Ponda aachiwe huru bila mashartiamesema kuanzia leo watu wote lazima wafuate sheria hukuakisisitiza kuhusu jambo hilo amesema 'mambo ya kutofuata sheria, mambo ya kudhani kuna wengine wako juu ya sheria yamepitwa na wakati kuanzia leo'

Amesema bwana Ponda atapewa dhamana na ndugu zake baada ya kufuata utaratibu wa sheria, amesisitiza kwamba kamwe jeshi la polisi halitamuachia eti kwa sababu ya mashinikizo kutoka kwa baadhi ya watu (nafikiri alikua anakumbuka mara ya mwisho walivomuachia bila masharti baada ya kupata shinikizo kutoka kwa waislamu)

Source: Radio One breaking news!