Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, October 20, 2012

VITA YA WENYEWE KWA WENYEWE TANZANIA!

NINI SULUHISHO YA HAYA YANAYOENDELEA TANZANIA YETU, NA NINANI WA KUSHOOSHEWA KIDOLE?. MUNGU IBARIKI TANZANIA



Askari Kanzu akimsindikiza kwa teke mmoja kati ya watuhumiwa waliokamatwa 
wakati wa operesheni maalum iliyowekwa katika jiji la Dar es Salaam,leo mchana ili kuwadhibiti 
baadhi ya waliodaiwa kuwa ni waumini wa dini ya kiislam, waliokuwa wamepanga kufanya 
maandano mchana wa leo baada ya Swala ya Ijumaa kuelekea Ikulu kwa lengo la kushinikiza 
kiongozi  wao, Katibu wa Jumuiya za Taasisi za Kiislam, Sheikh Ponda, aliyekamatwa majuzi,
aachiwe. 
Hata hivyo  jitihada za watu hao ziligonga ukuta baada ya wao kujipanga kutokea kila kona na 
kukutana maeneo ya Ikulu, lakini la Askari pia walijiandaa na kujipanga vyema kila kona ya jiji na kuwadhibiti watu hao. 
Vurugu kubwa ilikuwa katika maeneo ya Kariakoo ambako pia walijitokeza baadhi ya vijana aliojichanganya na makundi hayo na kuanza kuvamia maduka na kupora mali za watu na 
kuwatishia wenye maduka, jambo ambalo liliwafanya Polisi kuwatawanya kwa kupiga risasi hewani 
na waliokaidi amri hiyo walianza kushughulikiwa kama picha hizi zinavyoonyesha Pata Mkanda Kamili.

Twende garini.....

Akaaaa sio mimi jamaniiiiiii, Babu (kulia} akijitetea...

Askari wakimdhibiti babu...

Babu akishuhshwa garini kuingizwa kituoni.....

Mgambo wa kike akipambana na kijana kumburuta kumpeleka garini, 
baadaye mgambo huyu CHALIII

Mgambo chaliii, lakini wapi anaye tuuuu....

Watuhumiwa wakipandishwa garini....

Watuhumiwa wakipandishwa garini....

Watuhumiwa wakipandishwa garini....

Jamaa akijaribu kueskep ambapo alikula bonge la mtama na kutambaa kama hivi 
na kudakwa na mgambo wa kike....


 VIKOSI VYA USALAMA NA HALI YA VURUGU DAR ES SALAAM IJUMAA
Barabara ya kuingia katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya 
Nchi zikiwa zimefungwa na Askari Polisi kufuatia vurugu zilizotokea leo
Polisi wakifanya doria kwa kutumia pikipiki

 Mitaa ya Kariakoo na viunga vyake ikiwa imeimarishwa na Askari wa Jeshi
 la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika mitaa ya Kariakoo leo
 Ulinzi uliimarishwa na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika mitaa ya Kariakoo leo
 Wanajeshi wakivinjari katika mitaa ya Kariakoo leo
 Askari wa jiji wakishiriki kikamilifu katika zoezi la kuwakamata watu waliokuwa wamekusanyika 
kwa nia ya kutaka kuandamana katika eneo la Kariakoo
Magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa katika doria katika barabara ya 
Msimbazi ambako kulitokea vurugu zilizosababishwa na waislamu waliotaka kuandamana.
Watu hao walifika mmoja mmoja maeneo ya Ikulu kabla ya kudhibitiwa na Askari wa Kikosi 
cha Kutuliza Ghasia (FFU) na kupelekwa Kituo Kikuu cha Kati. Kukamatwa kwa watu hao kunafuatia
 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwatawanya waumini wa dini ya Kiislamu ambao walikuwa na nia ya kufanya maandamano.
Waandishi wameshuhudia gari mbili za jeshi la Polisi zikiwa zimebeba wanajeshi waliokuwa na silaha. Katika maeneo ya Kariakoo vikosi vya Jeshi la wananchi wa Tanzania vimekuwa vikifanya doria ili kuimarisha hali ya ulinzi.

MAGARI YA JESHI YALIVYOONGOZANA KWENDA KARIAKOO 

Hili ni moja ya Gari lililobeba wanajeshi ambao walikua doria wakati waandamaji 
waripoleta vurugu na kusababisha vurugu na mabomu ya machozi kulindima kwenye baadhi ya maeneo kama vile Kariakoo na Posta.Tuendeleee kuvuta subira...

Msafara wa magari ya JWTZ kuelekea tuliza Vurugu

Yakiwa yanaelekea eneo la Tukio

Picha hii ya Tamko kwa hisani ya Mo Blog

Endelea Kufuatilia


Picha zote kwa hisani ya Michuzi Blog


Chanzo: Vijimambo

No comments :

Post a Comment