Wawakilishi Wa CCM Watoa Tamko Kulaani Vurugu Zanzibar
Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Hamza Hassan CCM akifafanua jambo katika Kikao kilichofanywa na Wawakilishi wa CCM kutoa kauli ya Kulaani machafuko yanayoendelea ambayo yamesababisha kuchomwa Moto Maskani ya CCM ya Kisonge Mjini Zanzibar.
PICHA NA-MAKAME MSHENGA -MAELEZO ZANZIBAR
Wajumbe wa baraza la wawakilishi (ccm) wamelaani vikali vitendo vinavyoendelea kufanywa na jumuiya ya mwamsho kwa kuvunja amani, utulivu na kusababisha vurugu katika mji wa zanzibar kuanzia jana.
Hapo jana kundi la mwamsho lilivamia nyumba za watu maduka na kupora bidhaa kadhaa katika maduka na kusababisha hasara kubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari huko mbweni kwenye ukumbi wa baraza la wawakilishi, mhe. Hamza Hassan Juma kwaniaba ya wawakilishi wa Ccm amesema wakati umefika kwa serikali kuchukuwa hatua zinazofaa kabla hali haijawa mbaya zaidi.kwani kuendelea kukaa kimya kwa Serikali kutatoa sura mbaya kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari huko mbweni kwenye ukumbi wa baraza la wawakilishi, mhe. Hamza Hassan Juma kwaniaba ya wawakilishi wa Ccm amesema wakati umefika kwa serikali kuchukuwa hatua zinazofaa kabla hali haijawa mbaya zaidi.kwani kuendelea kukaa kimya kwa Serikali kutatoa sura mbaya kwa wananchi.
Amesema serikali imeunda serikali ya umoja wa kitaifa ili kuondoa kasoro zilizokuwepo na kuwafanya wananchi kuishi kwa amani na usalama na kuweza kuondoa tofauti zao za kisiasa. Amesema isifike pahala Zanzibar ikawa kama zile nchi zenye machafuko na kuwafanya wanachi wake kushindwa kuishi kwa amani na salama. Hivyo wajumbe hao waliitaka serikali mara moja kuwachukulia hatua wale wote ambao wamehusika na ghasia hizo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Aidha wamemtaka mkuu wa Jeshi la Polisi IGP na makamanda wenzake kuwajibika moja kwa moja juu ya suala hili ili kukomesha mambo hayo. Halkadhalika wajumbe hao waliitaka serikali kulipa fidia mali zote zilizoharibiwa kutokana na fujo hizo na kuviruhusu vikosi vya smz vkusaidia katika kuweka ulinzi na usalama ili maafa zaidi yasije yakatokea.
Akizungumzia suala la kufutwa jumuiya hiyo, Mhe. Hamza amesema jumuiya ya mwamsho si chama cha siasa ni jumuiya ya kidini lakini imeonekana kukosa muelekeo na kufanya vitendo vinavyowafarakanisha waumini wa dini hiyo, kuwagawa. na kuidhalilisha dini yenyewe ya kiislam.
Hivyo waliitaka taasisi inayohusika kuifuta Jumuiya hiyo kwa vile inakwenda kinyume na malengo na dhamira ya kuanzishwa kwake. Kuhusu kutoweka kwa Sheikh Farid, Mhe. Hamza amesema hadi hivi sasa haijulikani wapi alipo na nani aliyeyemchukuwa au kumteka nyara kwa vile kwa mara ya mwisho inasemekana alikuwa na dereva wake.
Wajumbe hao leo waligoma kuingia katika baraza wakilaani kitendo hicho na kusema kwamba kesho watapeleka hoja binafsi kwa spika wa baraza hilo ili kujadiliwa suala mwamsho na vitendo vyake dhidi ya serikali .
Chanzo: Wote Pamoja
No comments :
Post a Comment