KAULI YA ZAWA UK JUU YA VURUGU ZANZIBAR
ambayo yanaendelea kutokea huko nyumbani Zanzibar yaliyoanza
kujitokeza jana tarehe 17/10/2012 ambayo yamesababisha vurugu kubwa
katika Miji ya Zanzibar na vitongoji vyake.
Matukio hayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa maisha ya askari wa
jeshi la polisi,mali za Umma, wananchi mmoja mmoja na hata vyama vya
siasa. Miongoni mwa vitendo hivyo ni kuvunjwa Maduka, vyombo vya
usafiri, kukatwa miti ovyo na nguzo za umeme, pamoja na kuchomwa moto
maskani za CCM.
Kutokana na vitendo hivyo, ZAWA UK kinaalaani vikali matukio hayo
ambayo yamepelekea uvunjifu wa mkubwa wa amani ya nchi, na kusababisha
hofu kubwa kwa raia pamoja na wageni wanaotembelea Zanzibar.
Pamoja na vurugu hizo, ZAWA UK kimepokea kwa mshangao mkubwa taarifa
ya Serikali ya Zanzibar pamoja na ile ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano kupitia jeshi la Polisi iliyoeleza juu ya kutoweka kwa Sheikh
Farid Hadi Ahmed katika mazingira ya kutatanisha.
Katika Taarifa hiyo, Serikali zimethibitisha kuwa vyombo vyake vyote
vya ulinzi havijamkamata Sheikh Farid, jambo ambalo limezidisha hofu
na wasi wasi kwa wananchi juu ya mahali alipo na hali yake kiongozi
huyo wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar.
ZAWA UK kinaziomba Serikali zote mbili kuendeleza juhudi zote za
kuhakikisha taarifa za ukweli na za uhakika zinapatikana juu ya kadhia
ya kutoweka kwa Sheikh huyo kwani Sheikh Farid ni raia wa nchi hii, na
Serikali hii ni kwa ajili ya wananchi wote, ili kuondoa hofu na wasi
wasi ambao umesababisha baadhi ya wananchi kujengwa na dhana mbaya.
Vile vile ZAWA UK kinawaomba wananchi wote kwa ujumla kutojiingiza na
kutofanya vitendo vyovyote vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani ya
nchi yetu.
Sote kwa pamoja tukatae kabisa kujihusisha na vitendo vya kuleta
vurugu kwa vitendo na kauli zitakazopelekea kuiondolea sifa njema nchi
hii ya Zanzibar.
Mwenyekiti ZAWA UK
Hassan Mussa Khamis
No comments :
Post a Comment